Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Lebron na mwanaye waweka rekodi mpya NBA

Muktasari:

  • Bronny alizua gumzo baada ya kuchaguliwa kutoka katika drafti namba mbili la wachezaji akiwa chaguo la 55 na anatarajiwa kucheza kwenye ligi ndefu pamoja na baba yake kwenye timu hiyo.

REKODI mpya imewekwa kwenye mchezo wa mpira wa kikapu duniani, na hii imetokea kwenye Ligi ya NBA, baada ya juzi Ijumaa, Los Angeles Lakers kumtambulisha kikosini mtoto wa nyota wa timu hiyo, LeBron James aitwaje, Bronny James kama mchezaji mpya wa timu hiyo msimu ujao.

Bronny alizua gumzo baada ya kuchaguliwa kutoka katika drafti namba mbili la wachezaji akiwa chaguo la 55 na anatarajiwa kucheza kwenye ligi ndefu pamoja na baba yake kwenye timu hiyo.

Kutokana na hilo, ni wazi sasa LeBron ataendelea kucheza kwenye timu hiyo baada ya siku za nyuma kudai ana ndoto ya siku moja acheze timu moja na mwanaye kabla hajastaafu na sasa ataongeza mkataba wa miaka mitatu zaidi ya kuichezea timu hiyo.

Bronny kwa sasa ana umri wa miaka 19 wakati LeBron anaenda kucheza NBA msimu wa 22, hivyo inaenda kuwa rekodi ya muda wote kwa ligi hiyo kwa mchezaji mmoja kucheza na mwanaye timu moja.


RAUNDI YA PILI YA BRONNY

Wakati Bronny akichaguliwa namba 55, waliomtangulia mwanzoni kuanzia namba 31 ni Raptors kwa Jonathan Mogbo, Jazz kwa Kyle Filipowski, Bucks kwa Tyler Smith, Trail Blazers kwa Tyler Kolek aliyepelekwa Knicks, Spurs kwa Johnny Furphy akapelekwa Pacers, Pacers kwa Juan Nunez aliyepelekwa Spurs, Timberwolves kwa Bobi Klintman wakampeleka Pistons.

Knicks kwa Ajay Mitchell akapelekwa Thunder, Grizzlies kwa Jaylen Wells, Trail Blazers kwa Oso Ighodaro wakampeleka Suns kupitia Knicks, 76ers kwa Adem Bona, Hornets kwa KJ Simpson, Heat kwa Nikola Djurisic na kumpeleka Hawks, Rockets kwa  Pelle Larsson na kumpeleka Heat, Kings kwa Jamal Shead na Rockets.

Clippers kwa Cam Christie, Magic kwa Antonio Reeves  na kupelekwa Pelicans, Spurs kwa Harrison Ingram, Indiana Pacers  kwa Tristen Newton, Pacers kwa Enrique Freeman, Knicks kwa Melvin Ajinca na kupelekwa Mavericks, Warriors kwa Quinten Post na anapelekwa Thunder, Blazers na kuishia Warriors, Pistons kwa Cam Spencer na kupelekwa Grizzlies,  Celtics kwa Anton Watson, Suns kwa Kevin McCullar Jr na kupelekwa Knicks, Grizzlies kwa Ulrich Chomche anayeingia Raptors, Mavericks kwa Ariel Hukporti kupelekwa Knicks.


UFARANSA NAMBA MOJA TENA

BAADA ya mwaka jana, Victor Wembenyama kuchaguliwa namba moja kwenye draft na San Antonio Spurs, mwaka huu tena imejirudia kwa mchezaji raia wa Ufaransa kuchaguliwa kama namba moja, awamu hii akichaguliwa na Atlanta Hawks.

Zaccharie Risacher alifungua pazia la namba moja kwenda Hawks na waliofuata kwenye orodha hiyo na timu zao ni Washington Wizards waliomchagua Alex Sarr, Houston Rockets kwa Reed Sheppard, San Antonio Spurs kwa Stephon Castle,  Detroit Pistons kwa Ron Holland II na Charlotte Hornets kwa Tidjane Salaun .

Portland Trail Blazers kwa Donovan Clingan, Spurs tena kwa Rob Dillingham aliyepelekwa Minnesota Timberwolves, Memphis Grizzlies kwa Zach Edey, Utah Jazz kwa Cody Williams,  Chicago Bulls kwa Matas Buzelis, Oklahoma City Thunder kwa Nikola Topic na Sacramento Kings kwa Devin Carter.

Trail Blazers tena kwan Bub Carrington waliyempeleka Wizards, Miami Heat kwa Kel’el Ware, Philadelphia 76ers kwa Jared McCain, Los Angeles Lakers kwa Dalton Knecht, Orlando Magic kwa Tristan da Silva, Toronto Raptors kwa Ja’Kobe Walter,  Clevaland Cavaliers kwa Jaylon Tyson,  New Orleans Pelicans kwa Yves Missi.

Phoeniz Suns kwa DaRon Holmes II aliyeenda Denver Nuggets, Milwaukee Bucks kwa AJ Johnson,  New York Knicks kwa Kyshawn George wa Miami aliyepelekwa Wizards, Knicks kwan Pacome Dadiet, Wizards kwa Dillon Jones aliyepelekwa kwa OKC Thunder, Timberwolves kwa Terrence Shannon Jr, Nuggets kwa Ryan Dunn aliyepelekwa Suns, Jazz kwa Isaiah Collier na Celtics kwa Baylor Scheierman.