Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Lando Norris awatega Mclaren

Muktasari:

  • Norris ambaye yupo nyuma ya Max Verstappen kwenye mbio za ubingwa wa jumla wa mbio za magari duniani, alisema wazi anahitaji maboresho ya gari za kampuni hiyo aliyoyaita yasiyo sawa na yalichangia kumwangusha kwenye mbio zilizopita.

KAMA sio kuangushwa na gari za kampuni yake McLaren, dereva Mwingereza, Lando Norris anaamini angefanya vyema zaidi ya ilivyotokea kwenye mbio mbili zilizopita hususan ile ya mwisho ya Ubelgiji.

Norris ambaye yupo nyuma ya Max Verstappen kwenye mbio za ubingwa wa jumla wa mbio za magari duniani, alisema wazi anahitaji maboresho ya gari za kampuni hiyo aliyoyaita yasiyo sawa na yalichangia kumwangusha kwenye mbio zilizopita.

Hilo limemfanya bosi wa kampuni hiyo, Andrea Stella kukubali madai ya dereva huyo na wanafanya kila wawezalo ili mbio zikirudi kutoka mapumziko ya takribani mwezi, watakuwa wameboresha kama Norris alivyolalamikia gari zao.