Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kwa maneno haya... Salah anasepa!

Muktasari:

  • Kwa mambo yalivyo kwa sasa, staa huyo wa Misri anajiandaa kuondoka bure kwenye kikosi hicho cha Anfield kutokana na mkataba wake kufika ukingoni mwishoni mwa msimu.

LIVERPOOL, ENGLAND: SUPASTAA, Mohamed Salah ameweka mambo haradhani huu unaweza kuwa msimu wake wa mwisho kwenye kikosi cha miamba ya soka ya Anfield, Liverpool.

Kwa mambo yalivyo kwa sasa, staa huyo wa Misri anajiandaa kuondoka bure kwenye kikosi hicho cha Anfield kutokana na mkataba wake kufika ukingoni mwishoni mwa msimu.

Salah amekuwa kwenye kiwango bora sana msimu huu akiifanya Liverpool kuongoza msimamo wa Ligi Kuu England kwa tofauti ya pointi 13 dhidi ya Arsenal inayoshika nafasi ya pili.

Amehusika katika mabao 42 kwenye Ligi Kuu England, akifunga 25 na kuasisti 17, takwimu zinazomweka kocha mpya wa kikosi hicho, Arne Slot kwenye nafasi nzuri ya kubeba taji katika msimu wake wa kwanza.

Lakini, sasa inavyoonekana namba hizo hazitoshi kumfanya aendelee kubaki Anfield kwa zaidi ya msimu huu.

Mo Salah alizungumza na gwiji wa Liverpool, Steve McManaman kuhusu nyakati zake kwenye kikosi cha Liverpool kabla ya mchezo wa usiku wa Jumatano dhidi ya Newcastle United uwanjani Anfield.

Salah, 32, kwa sasa ndiye mchezaji anayeshika namba tatu kwa kuwa kinara wa mabao wa muda wote kwenye historia ya klabu ya Liverpool. Salah ni kama alikuwa akizungumza kwa lugha ya yaliyopita, lakini kitu ambacho mashabiki wanapaswa kukifahamu ni kwamba siku za staa huyo Liverpool zinahesabika.

Mo Salah alisema: “Nataka mashabiki wakumbuke kwamba ninachokifanya ni kwa ajili yao kwa ajili ya jiji hili. Nilipokuwa hapa, sikuwa mvivu, nilifurahia soka langu na kujitolea kila kitu.

“Nadhani hicho ndicho kinachohitajika kwenye hili jiji, wanakupenda, unapaswa kuungana nao. Nataka wakumbuka nilipokuwa hapa kwa miaka minane au vinginevyo.”

McManaman kisha alimuuza Mo Salah kama mashabiki wa Liverpool watahitaji abaki kwa zaidi ya miaka hiyo minane aliyokuwa kwenye timu, mkali huyo wa zamani wa FC Basel, Chelsea, AS Roma na Atalanta alijibu kwa kusema: “Hapana, katika sauti ya utulivu.”

Kwa sasa Mo Salah yupo huru kuzungumza na klabu yoyote ya ng’ambo na kusaini mkataba wa awali na kuna timu kibao zinahitaji huduma yake, ikiwamo za Saudi Arabia. Hii ni mara ya tano kwa Mo Salah kuweka wazi atakwenda kuachana na Liverpool mwishoni mwa msimu huu.

Salah alifunga bao lake la 241 Jumapili iliyopita na kulingana na gwiji Gordon Hodgson kwa mabao. Ian Rush ndiye kinara wa mabao wa muda wa Liverpool, akifunga 346 na kufuatiwa na Roger Hunt, aliyetikisa nyavu mara 285.