Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kumbe Raha za Yamal zingekuwa Bayern sasa

Muktasari:

  • Yamal, mwenye umri wa miaka 18, aling’ara katika kikosi cha kwanza cha Barca mwaka 2023 akiwa na umri mdogo wa miaka 15, miezi 9 na siku 16 tu.

BARCELONA, HISPANIA: INAWEZEKANA akawa ndio mchezaji anayependwa sana na mashabiki wa Barcelona kwa sasa, lakini Lamine Yamal alikuwa karibu kutimkia kwa vigogo wengine barani Ulaya kabla ya dili kufeli na kusalia Barca.

Yamal, mwenye umri wa miaka 18, aling’ara katika kikosi cha kwanza cha Barca mwaka 2023 akiwa na umri mdogo wa miaka 15, miezi 9 na siku 16 tu.

Tangu wakati huo, winga huyo amecheza mechi 109 za michuano yote, akifunga  mabao 27 na kutoa asisti 37.

Tayari ameshashinda mataji mawili ya La Liga na kombe moja la Copa del Rey akiwa na miamba hiyo ya Catalunya, na pia alishinda taji la Euro 2024 akiwa na timu ya taifa ya Hispania.

Kwa mujibu wa gazeti la Bild, Yamal alikaribia kujiunga na Bayern Munich mwaka 2022 akiwa na umri wa miaka 14 tu.

Bayern ilifanya jitihada kubwa kumsajili baada ya viongozi wa klabu kuonyeshwa video zake na idara ya maskauti ambao kwa wakati huo, walikuwa pia wanamfuatilia Gavi aliyekuwa sambamba na Yamal.

Mkurugenzi wa michezo wa Bayern, Hasan Salihamidzic pamoja na mkurugenzi wa ufundi Marco Neppe walizungumza na wakala wa Yamal wa wakati huo, aliyekuwa ni nyota wa zamani wa Barca, Ivan de la Pena, ili kuona kama wanaweza kuipata huduma ya kinda huyo.

De la Pena aliwajulisha Bayern kuwa atazungumza na familia ya Yamal kuhusu hilo, lakini dili hilo lisingeweza kukamilika hadi Julai 13, 2023, pale mchezaji huyo alipokuwa akifikisha umri wa miaka 16.

Lakini mambo yalibadilika ghafla baada ya Yamal kusaini mkataba na wakala mwingine Jorge Mendes ambaye pia alizungumza na Bayern na kuijulisha kuwa ingelazimika kutoa kiasi cha takribani Pauni 4.3 milioni ili kuishawishi familia ya kijana huyo kuhamia na mchezaji jijini Munich.

Lakini viongozi wa Bayern walichelewa kufanya uamuzi kuhusu kama walikuwa tayari kutoa fedha nyingi kiasi hicho kwa kijana mdogo na hivyo dili likafa.

Yamal ambaye alijiunga na akademi ya Barcelona akiwa na umri wa miaka sita alicheza mechi yake ya kwanza kwenye kikosi cha kwanza Aprili 2023, akiwa na umri wa miaka 15, miezi 9 na siku 16.