Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kumbe kipa Grimsby imemuuma sana

KIPA Pict

Muktasari:

  • Hata hivyo, kipa huyo amefichua kwamba yeye ni shabiki wa Man United, hivyo alikasirishwa na matokeo hayo, ambapo Grimsby ilishinda kwa kwa mikwaju ya penalti 12-11 baada ya sare ya mabao 2-2 katika muda wa kawaida.

LONDON, ENGLAND: KIPA wa Grimsby Town, Christy Pym amewashangaza mashabiki kwa namna alivyokuwa akishangilia baada ya kuitupa nje Manchester United kwenye Kombe la Ligi, lakini kumbe jambo hilo limemuuma sana.

Hata hivyo, kipa huyo amefichua kwamba yeye ni shabiki wa Man United, hivyo alikasirishwa na matokeo hayo, ambapo Grimsby ilishinda kwa kwa mikwaju ya penalti 12-11 baada ya sare ya mabao 2-2 katika muda wa kawaida.

Pym, 30, ambaye aliokoa hatari kadhaa katika mechi hiyo ikiwamo kwenye tukio la kupigiana penalti, ambapo alidaka mkwaju wa Matheus Cunha.

Licha ya ushindi huo, kipa huyo alisema hakuwa na furaha sana kwa sababu alikuwa kwenye njia panda, Man United ni timu yake anayoshabiki.

Alisema: "Mimi ni shabiki wa Man United, hivyo nimechukia kiasi. Usiku kama huu ndio unaofanya tucheze soka. Ningeweza kufanya vizuri zaidi, sivyo?

"Niliokoa penalti moja ili timu iwepo mchezoni na vijana walifanya walichobaki."

Pym alitua Blundell Park mwezi uliopita baada ya kusaini dili la miaka miwili akiwa mchezaji huru baada ya kuachana na Mansfield Town kwenye dirisha hili.

Kipa huyo aiwahi kuwa kwenye akademia ya Man United na kucheza sambamba na Marcus Rashford na Scott McTominay. Hata hivyo, aliachwa 2019 na kwenda kucheza soka kwenye ligi za chini.

MECHI ZIJAZO ZA KOMBE LA LIGI MSIMU HUU

Port Vale vs Arsenal

Lincoln City vs Chelsea

Tottenham vs Doncaster

Huddersfield vs Man City

Liverpool vs Southampton

Fulham vs Cambridge

Brentford vs Aston Villa

Barnsley vs Brighton

Swansea vs Nottingham Forest

Newcastle United vs Bradford

Sheffield Wednesday vs Grimsby Town

Wolves vs Everton

Crystal Palace vs Millwall

Burnley vs Cardiff City

Wrexham vs Reading

Wigan vs Wycombe Wanderers