Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kuhusu Jude Bellingham sikia hii

JUDE

Muktasari:

  • Bellingham alikulia katika timu ya vijana ya klabu yake ya nyumbani, Birmingham City, kabla ya kuhamia Borussia Dortmund mwaka 2020 kwa ada ya awali inayoripotiwa kuwa Pauni 25 milioni.

LONDON,ENGLAND: STAA wa Real Madrid, Jude Bellingham ameweka wazi juu ya uwezekano wa kucheza Ligi Kuu England, baada ya ripoti kudai kuwa mchezaji huyo wa kimataifa wa Real Madrid anaweza akatua katika ligi hiyo.

Bellingham alikulia katika timu ya vijana ya klabu yake ya nyumbani, Birmingham City, kabla ya kuhamia Borussia Dortmund mwaka 2020 kwa ada ya awali inayoripotiwa kuwa Pauni 25 milioni.

Kiungo huyo alidumu kwa misimu mitatu katika klabu hiyo ya Bundesliga kabla ya kuhamia Madrid katika dirisha la majira ya kiangazi mwaka 2023 kwa ada ya awali ya uhamisho inayoripotiwa kuwa kufikia Euro 103  milioni.

Hadi sasa akiwa katika viunga vya Santiago Bernabeu, Bellingham ameshinda taji la La Liga, Ligi ya Mabingwa Ulaya, Supercopa de Espana, UEFA Super Cup na FIFA Intercontinental Cup.

JUD 01

Bellingham pia amecheza mechi 46 za timu ya taifa ya  na kufunga mabao sita, akiwa sehemu ya kikosio cha taifa hilo kilichomaliza nafasi ya pili katika Euro 2020 na Euro 2024, na kufika robo fainali za Kombe la Dunia mwaka 2022 nchini Qatar.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23 bado hajacheza Ligi Kuu  England, ingawa alicheza katika Championship akiwa na Birmingham ambapo alifunga mabao manne katika michezo 44 ya mashindano yote.

Baada ya kucheza katika ligi kuu za Ujerumani na Hispania, bado kuna swali la kama atacheza Ligi Kuu ya England siku za usoni.

Hivi karibuni, ripoti zimedai  kuwa iwapo Cole Palmer atarejea katika klabu yake ya zamani, Manchester City, basi Chelsea inaweza kutaka kumsajili Bellingham ili akachukue nafasi yake.

Hata hivyo, uhamisho huo haonekani kuwa rahisi kutokana na ukweli kwamba Madrid haipo tayari kumuuza staa huyo kwa sasa.

JUD 02

Hta hivyo, dili hilo pia linaonekana kuwa ni kinyume na sera ya uhamisho ya Chelsea katika miaka ya hivi karibuni, ambayo imekuwa ikisajili  wachezaji wadogo inaoweza kuwaendeleza badala ya wale waliokoma tayari.

Sababu nyingine inayofanya uwezekano wa uhamisho huo kuwa mdogo ni mawazo ya Bellingham mwenyewe kuhusu kucheza Ligi Kuu England, ambapo alithibitisha kuwa hakuwa na mpango huo.

Akizungumza Oktoba 2023 na Channel 4, Bellingham amesema anataka kubaki Santiago Bernabeu walau kwa miaka kumi na labda hadi 15, jambo linaloweza kumfanya akae hapo hadi anastaafu.

Vilevile, Kupitia Evening Standard, Bellingham amesema:"Hii ndiyo klabu ninayotaka kuwa nayo kwa miaka 10 hadi 15 ijayo ya maisha yangu. Ninafurahia sana kuwa hapa."