Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

He! Alonso akalia kuti kavu Madrid

Muktasari:

  • Real Madrid imekuwa kwenye wakati mgumu chini ya kocha Alonso, 44, baada ya Jumapili iliyopita kutoka sare ya 1-1 dhidi ya Girona kwenye LaLiga.

MADRID, HISPANIA: KOCHA wa Real Madrid, Xabi Alonso anakabiliwa na hatari ya kufutwa kazi kwenye klabu hiyo endapo matokeo na kiwango cha timu vitashindwa kuwa vizuri kwa haraka.

Real Madrid imekuwa kwenye wakati mgumu chini ya kocha Alonso, 44, baada ya Jumapili iliyopita kutoka sare ya 1-1 dhidi ya Girona kwenye LaLiga.

Los Blancos sasa imetoka sare kwenye mechi zao tatu zilizopita kwenye ligi baada ya mechi za Rayo Vallecano na Elche. Real Madrid iliichapa Olympiacos 4-3, Jumatano iliyopita kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya, lakini katika mechi hiyo ilishuhudia ikiwa kwenye hali mbaya katika dakika 10 za mwisho za kipute hicho cha Ugiriki.

Ripoti zinafichua kwamba kocha Alonso sasa yupo kwenye wakati mgumu kutokana na matokeo hayoya mabovu, ambapo ushindi wa Real Madrid wa hivi karibuni kwenye ligi ulikuwa Novemba 1 iliposhinda 4-0 dhidi ya Valencia uwanjani Santiago Bernabeu.

Kuna taarifa zinafichua kwamba mechi zijazo za Real Madrid zitabeba uamuzi mkubwa wa mabosi wa Real Madrid bila shaka watahitaji matokeo mazuri na kiwango cha ushawishi. Real Madrid ilianza msimu kwa kasi sana chini ya Alonso kwenye LaLiga ambapo ilishinda mechi 10 kati ya 11 za kwanza. Lakini, baada ya hapo mambo yaligeuka, hasa baada ya Vinicius Jr kutokuwa na furaha kwenye timu na kutupwa benchini.

Kocha Alonso bado anashindwa kupata uwiano mzuri kwenye kikosi kwa kuwapanga kwa pamoja Kylian Mbappe, Vinicius na Jude Bellingham. Na kinachoelezwa ni kwamba kuna wachezaji wasiopungua sita wamekuwa hawana furaha na uongozi wa kocha Alonso.

Kundi hilo lenye wachezaji wasiomkubali Alonso kuna mastaa kama Fede Valverde, Vinicius, Rodrygo, Brahim Diaz, Endrick na Ferland Mendy. Real Madrid kwa sasa inashika nafasi ya pili kwenye msimamo wa LaLiga, ikizidiwa pointi moja na vinara Barcelona.