Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kocha Super Eagles ajutia kauli yake, awaomba radhi DR Congo

CHELLE Pict

Muktasari:

  • Nigeria ilipoteza kwa penalti 4-3 dhidi ya Leopards katika mechi ya fainali ya kufuzu Kombe la Dunia 2026, Jumapili, Novemba 16, 2025 kwenye Uwanja wa Adrar, Agadir nchini Morocco.

Kocha mkuu wa timu ya taifa ya Nigeria maarufu Super Eagles, Eric Chelle, ameomba radhi kwa wachezaji na maafisa wa DR Congo baada ya kutoa maneno ya shutuma za ‘uchawi’ ilipomalizika mechi ya fainali ya mchujo wa kufuzu Kombe la Dunia 2026.

Nigeria ilipoteza kwa penalti 4-3 dhidi ya Leopards katika mechi ya fainali ya kufuzu Kombe la Dunia 2026, Jumapili, Novemba 16, 2025 kwenye Uwanja wa Adrar, Agadir nchini Morocco.

Mechi hiyo ilimalizika kwa sare ya bao 1-1 ndani ya dakika 120, ambapo Mechak Elia aliisawazisha DR Congo baada ya Frank Onyeka kuitanguliza Nigeria.

Calvin Bassey, Moses Simon, na Semi Ajayi wote walikosa penalti kwa Super Eagles, huku Chelle akilishutumu benchi la ufundi la DR Congo.

Baada ya mechi hiyo iliyokuwa na upinzani mkali, Chelle aliwaambia waandishi wa habari kwamba, mtu fulani katika benchi la ufundi la DR Congo alikuwa akifanya vitendo vya ‘uchawi’ wakati wa mapigo ya penalti.

Hata hivyo, kocha huyo ametumia muda wake kutafakari na amekiri kukosea kwa kauli hiyo, jambo ambalo limemfanya kuwasilisha maneno yake ya kuomba radhi kupitia ukurasa wake wa Instagram.

Kocha huyo raia wa Mali ameandika: “Soka ni mchezo wa hisia. Baada ya mechi, nilionyesha vitendo vilivyochochewa na hasira kwa kuibua mzozo na maofisa benchi la ufundi la DR Congo, baada ya kuhisi kuna mtu akijaribu kuingia kwenye eneo langu la kiufundi.

"Hapo nyuma sijawahi kumkashifu mtu yeyote wa DR Congo au wafanyakazi wao ambao ninawaheshimu. Nimekasirika kwa kutolewa kwetu lakini najivunia wachezaji wangu. Hongera kwa DR Congo, ambayo ilikuwa bora zaidi yetu.
Mashabiki wao walionyesha shauku kubwa kama ilivyokuwa kwetu. Tushirikiane kwa ajili ya mambo yajayo yajayo.”