Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kocha Super Eagles aishutumu DR Congo kwa ‘uchawi’

UCHAWI Pict

Muktasari:

  • Chelle ametoa madai hayo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari baada ya mechi hiyo, akisema kuwa hasira zake zilielekezwa kwa baadhi ya wahudumu wa benchi la DR Congo wakati wa tukio hilo la penalti lililokuwa na mvutano mkubwa.

Kocha mkuu wa timu ya taifa ya Nigeria, Eric Chelle, ameishtumu DR Congo kwa kutumia ‘uchawi’  wakati wa mikwaju ya penalti katika mechi ya fainali ya mchujo wa kufuzu Kombe la Dunia 2026, iliyochezwa nchini Morocco jana Jumapili, Novemba 16, 2025.

Chelle ametoa madai hayo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari baada ya mechi hiyo, akisema kuwa hasira zake zilielekezwa kwa baadhi ya wahudumu wa benchi la DR Congo wakati wa tukio hilo la penalti lililokuwa na mvutano mkubwa.

Nigeria ilipata bao la mapema dakika ya tatu kupitia shuti la Frank Onyeka lililomgonga beki wa DR Congo na kuingia wavuni, kabla ya Meschak Elia kuisawazishia DR Congo baadaye katika kipindi cha kwanza. 

Hata hivyo, timu hizo zilimaliza dakika 120 zikifungana bao 1-1, hali ambayo ilipelekea sheria ya mikwaju ya penalti kuchukua mkondo wake, na ndipo Nigeria ilipong'olewa kwenye mchakato wa kufuzu Kombe la Dunia 2026.

Baada ya Chancel Mbemba kufunga penalti ya ushindi, Chelle alikimbilia eneo la benchi la DR Congo na kukabiliana na baadhi ya wafanyakazi wao, akiwemo kocha mkuu Sébastien Desabre, kabla ya kuzuiwa na maofisa wa Nigeria.

Desabre, ambaye alizungumza kwanza katika mkutano wa wanahabari baada ya mechi, alipuuzia tukio hilo na kusema kwamba si jambo kubwa.

Hata hivyo, Chelle hakukubaliana naye, kwa kusema kuwa baadhi ya watu wa benchi la DR Congo walikuwa wakifanya ‘mila za uchawi’ wakati wa kila mkwaju wa penalti na kudai kuwa alimwona mtu katika benchi lao akitumia ‘kitu kama maji’ ili kuwachanganya wachezaji wa Nigeria.

“Katika kila kipindi cha penalti, yule jamaa wa DR Congo alikuwa akifanya ‘uchawi’, alifanya hivyo kila wakati, na ndiyo maana nilikuwa na hasira kidogo dhidi yake,” amesema Chelle.

Alipoulizwa alichoona yule mtu akifanya, Chelle ameongeza: “Ndiyo, kitu kama… sijui kama ni maji au kitu kama hicho, alikuwa anakinyunyiza juu.”

Kichapo hicho kimesitisha safari ya Nigeria kufuzu Kombe la Dunia 2026, ikiendelea katika mkwamo huo kama ilivyokuwa mwaka 2022.

Hii ni ni mara ya kwanza kwa Nigeria kukosa kushiriki Kombe la Dunia mara mbili mfululizo tangu walipoanza kushiriki kwa mara ya kwanza mwaka 1994 nchini Marekani.