Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kocha Spurs akalia kuti kavu, wakati wowote kitanuka

SPURS Pict

Muktasari:

  • Kwa sasa, mpango wao ni Frank kuiongoza timu katika mechi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Borussia Dortmund Jumanne kisha baada ya hapo kutafanyika tathmini ikiwa anaweza kuendelea au afungashiwe virago.

LONDON, ENGLAND: MUSTAKABALI wa Kocha Thomas Frank katika kikosi cha Tottenham uko matatani baada ya mashabiki kutaka afukuzwe baada ya kipigo cha nyumbani cha mabao 2-1 kutoka kwa West Ham.

Taarifa ya Daily Mail inadai klabu hiyo ya Kaskazini mwa London inafikiria kufanya mabadiliko ya kocha, ingawa bado siyo kwa haraka.

Kwa sasa, mpango wao ni Frank kuiongoza timu katika mechi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Borussia Dortmund Jumanne kisha baada ya hapo kutafanyika tathmini ikiwa anaweza kuendelea au afungashiwe virago.

Kabla ya mechi dhidi ya West Ham taarifa zilieleza Frank alikuwa anaungwa sana mkono na viongozi wa klabu na hakukuwa na mpango wa kumfukuza.

SPU 01

Hata hivyo, kutokana na hali ya hasira kutoka kwa mashabiki iliyoonekana uwanjani baada ya Tottenham kufungwa bao la dakika ya 93, inaelezwa klabu sasa inafikiria kuita kikao cha bodi ili kujadili hatma yake wiki hii.

Wiki iliyopita, Spurs ilimwajiri John Heitinga kama kocha msaidizi na za ndani zinadai ndiye anaweza akachukua mikoba ya kuiongoza timu hiyo kwa muda ikiwa Frank ataondoka.

Tottenham kwa sasa ipo nafasi ya 14 kwenye msimamo wa Ligi Kuu England na katika mechi nane zilizopita za mashindano yote imeshinda moja tu.

SPU 02

Wakati Spurs ikiwa inaongozwa mashabiki walisikika wakiimba kocha afukuzwe asubuhi ya siku inayofuata kwa sababu ya mwenendo mbaya wa timu.

Baada ya mchezo, Frank amesema: "Katika maisha yangu ya ukocha, nimewahi kuwa na nyakati bora, nakiri kwa kusema huu si wakati mzuri kwangu. Lakini ninaelewa, mimi ndiye mtu aliyepewa dhamana. Hivyo lawama zitanielekea mimi. Hilo ni sawa, sina tatizo na hilo. Ilimradi mashabiki wanaendelea kuwaunga mkono wachezaji, kufanya kila wawezalo kuwasaidia na kuwasukuma waende mbele, ndivyo tunavyofanya nasi tutaendelea kusonga mbele."

SPU 03

“Hii ni kama meli kubwa sana na tunapambana kuigeuza kuelekea mwelekeo sahihi na kuna dalili nyingi nzuri nyuma ya pazia na pia katika baadhi ya mechi, lakini unapofungwa dakika za mwisho na mpinzani wako, hisia hutawala na mashabiki lazima wataongea na kupiga kelele. Kelele hizo tunapaswa kuziacha nje, tuinue vichwa vyetu na kuendelea kufanya kazi."