Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kocha Chelsea kazi anayo

Muktasari:

  • Kocha huyo raia wa Italia anakuna kichwa kupambana na majukumu makubwa yanayomkabili kwa sasa ndani na nje ya uwanja ikiwemo ishu ya Enzo Fernandez ambaye alichafua hali ya hewa klabuni hapo.

LONDON, ENGLAND : KIKOSI cha Chelsea kilitua Marekani, Jumanne ya wiki iliyopita kwa ajili ya maandalizi ya msimu, lakini kikiwa huko, kocha wake, Enzo Maresca ana kazi kubwa.

Kocha huyo raia wa Italia anakuna kichwa kupambana na majukumu makubwa yanayomkabili kwa sasa ndani na nje ya uwanja ikiwemo ishu ya Enzo Fernandez ambaye alichafua hali ya hewa klabuni hapo.

Timu hiyo inadaiwa kugawanyika juu ya ishu hiyo ya Enzo na video iliyosambaa akiimba wimbo wa kibaguzi na wachezaji wenzake wa Argentina juu ya wachezaji wa Ufaransa wenye asili ya Afrika imetibua mambo Stamford Bridge na kocha huyu atatakiwa kufanya kazi ya ziada kurekebisha mambo ili kikosi kikae sawa.

Licha ya Enzo kuomba msamaha inaelezwa, wachezaji wenzake wanaotokea Ufaransa bado hawajamsamehe na hawahitaji hata kumuona.

Kingine kilichopo mbele yake ni ishu ya  beki wa kikosi hicho, Trevoh Chalobah ambaye hajasafiri na kikosi hicho akiachwa London na mashabiki wamekosoa na kumshambulia kocha huyo kwa maneno.

Mmoja kati ya mashabiki hao aliandika kupitia mtandao wa X(Twitter), “Trevoh Chalobah kutokuwepo katika kikosi chetu kilichokwenda Marekani ni moja ya mambo ambayo hayakubaliki, bado ana mkataba na timu hadi mwaka 2028, anaondoshwa katika timu licha ya kucheza mechi kibao msimu uliopita, hii sio njia sahihi ya kumfanyia mwanadamu ambaye amekuwa katika timu  tangu ana umri wa miaka nane.’’

Mbali ya mashabiki, kitendo cha kuachwa kwa Chalobah pia kimeripotiwa kuwachoma baadhi ya wachezaji ambao wameanza kuona kocha hafanyi sawa na hilo pia linaweza kutokea kwao kwani wanaamini staa huyo alijituma sana msimu uliopita.

Enzo atatakiwa kuweka sawa mambo baina ya wachezaji wake kuhusu suala la Enzo kisha hili la Chalobah wakati huo huo kusuka timu kwa ajili ya kufanya vizuri msimu ujao mambo ambayo atatakiwa kuyafanya ndani ya wiki tatu zilizosalia kabla ya ligi kuanza.