Calafiori aondoke? Hana huo mpango

Muktasari:
- Calafiori alijiunga na Arsenal kutokea Bologna wakati wa dirisha la majira ya kiangazi la mwaka jana, lakini ameshindwa kutamba sana kutokana na kusumbuliwa na majeraha.
LONDON, ENGLAND: BEKI wa Arsenal, Riccardo Calafiori ameweka wazi juu ya uvumi unaozagaa kuhusu ripoti kwamba anahusishwa na mpango wa kuachana na miamba hiyo ya Emirates.
Calafiori alijiunga na Arsenal kutokea Bologna wakati wa dirisha la majira ya kiangazi la mwaka jana, lakini ameshindwa kutamba sana kutokana na kusumbuliwa na majeraha.
Ripoti kutoka Italia zinadai kwamba Arsenal imefungua milango ya kumuuza beki huyo mwenye umri wa miaka 23 na klabu kama AC Milan na Juventus zinataka kumrudisha Serie A.
Hata hivyo, Calafiori sasa ameibuka na kuzima uvumi huo na kusema: “Nina furaha hapa Arsenal.”
Calafiori alisema pia hajutii juu ya uamuzi wake wa kuhamia kwenye klabu hiyo ya London Kaskazini, aliposema: “Kwangu mimi binafsi hii imenipa uzoefu mkubwa. Mara zote unaposhinda mataji zinakuwa nyakati bora. Hapa nimekuja kujipima dhidi ya umuhimu na ugumu wa ubingwa kwenye hii dunia. Najisikia vyema kwa nafasi ninayopangwa, najaribu kusaidia timu yangu.”
Calafiori huko nyuma aliwahi kukiri kwamba haikuwa rahisi kuzoea maisha ya Arsenal.