Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kocha Brentford afunguka ishu ya Toney

Muktasari:

  • Fowadi huyo Mwingereza mwenye umri wa miaka 28, amekuwa kwenye rada ya Manchester United na Chelsea, huku akihusishwa pia na mpango wa kutimkia huko Saudi Arabia.

LONDON, ENGLAND: STRAIKA, Ivan Toney hakupewa nafasi kwenye kikosi cha Brentford kilichokipiga na Crystal Palace kwenye mchezo wa Ligi Kuu England wikiendi iliyopita.

Fowadi huyo Mwingereza mwenye umri wa miaka 28, amekuwa kwenye rada ya Manchester United na Chelsea, huku akihusishwa pia na mpango wa kutimkia huko Saudi Arabia.

Na sasa kocha wa Brentford, Thomas Frank alikiri kwamba kukosekana kwa Toney kwenye kikosi kunatokana na mazungumzo yanayoendelea ya usajili wa mchezaji huyo.

Kocha Frank aliiambia Sky Sports: “Kuna mambo mengi yanayoendelea kuhusu Ivan, hasa kwenye usajili.

“Kuna timu zinavutiwa na huduma yake, hakuna dili lililokamilika, lakini mambo yanaweza kutokea muda wowote, hivyo hatukuona sababu ya kumweka kwenye kikosi.”

Mchezaji ambaye alinaswa kwa ajili ya kuja kuchukua mikoba ya Toney, staa Igor Thiago anasumbuliwa na maumivu ya goti na atakuwa nje ya uwanja hadi Krismasi mwaka huu. Thiago, 23, alijiunga na Brentford kwa ada ya Pauni 30 milioni akitokea Club Bruges kwenye dirisha hili la uhamisho wa majira ya kiangazi huko Ulaya.

Hata hivyo, hilo haliifanyi Brentford kufikiria kuzuia dili la Toney kuondoka kwenye timu hiyo katika dirisha hili. Arsenal, Tottenham, West Ham, Chelsea na Man United ni kati ya timu zilizoonyesha kuhitaji saini ya straika huyo, lakini mambo yameonekana kuwa magumu kutokana na bei anayouzwa, timu yake inahitaji Pauni 60 milioni.

Na sasa Man United na Chelsea zinataka kujaribu dili la kumnasa kwa mkopo, huku taarifa zikidai kwamba anaweza kutimkia Saudi Arabia kuvuna mapesa.