Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kiungo mpya alia kisa jezi ya Arsenal

Muktasari:

  • Staa huyo mpya aliyesajiliwa na Arsenal dirisha hili alipiga picha kwa mara ya kwanza akiwa ametinga uzi wa miamba hiyo ya Emirates, huku akimwona mwanaye pia akivaa jezi hiyo ya The Gunners ikiwa na jina lake mgongoni, kitu kilichomfanya ashindwe kuvulia na kumwaga machozi.

LONDON, ENGLAND: KIUNGO Christian Norgaard ameangua kilio kwa kushindwa kuamini baada ya kutinga uzi wa Arsenal sambamba na mwanaye wa kiume katika tukio la kupiga picha.

Staa huyo mpya aliyesajiliwa na Arsenal dirisha hili alipiga picha kwa mara ya kwanza akiwa ametinga uzi wa miamba hiyo ya Emirates, huku akimwona mwanaye pia akivaa jezi hiyo ya The Gunners ikiwa na jina lake mgongoni, kitu kilichomfanya ashindwe kuvulia na kumwaga machozi.

Norgaard, 31, alikamilisha uhamisho wake wa kujiunga na Arsenal akitokea Brentford dirisha hili la uhamisho wa majira ya kiangazi. Kwenye kikosi hicho cha Arsenal, kiungo huyo amekabidhiwa jezi yenye Namba 16 na kilichomtoa machozi ni baada ya kumwona mwanaye akiwa amevaa jezi za Arsenal juu na chini, huku ikiwa na jina la 'Norgaard 16' mgongoni.

Staa huyo wa Denmark alikwenda kumkumbatia kwa nguvu mwanaye, huku video ya tukio hilo ikionyesha kiungo huyo alikuwa hataki kumwachia mwanaye aondoke.

Mashabiki walikomenti baada ya picha na video yake kupostiwa mtandaoni na wa kwanza alisema: “Jamaa anaonekana ni mtu wa viwango.” Na mwingine aliongeza: "Ni kitu spesho kuona ndoto zimetimia. Atalia zaidi atakaposikia wimbo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa mara ya kwanza.”

Shabiki wa tatu alisema: “Hiyo ndo maana yake. Ndivyo ilivyo. Karibu kwenye familia.”

Norgaard alikuwa mchezaji muhimu kwenye kikosi cha Brentford tangu alipojiunga akitokea Fiorentina mwaka 2019. Lakini, baada ya kocha Thomas Frank kuhamia Tottenham, Norgaard ni mmoja wa wachezaji ambao pia wameamua kuachana na Brentford kwenda kutafuta changamoto mpya.

Arsenal ilikubali kulipa ada ya Pauni 15 milioni kunasa saini ya mchezaji huyo, ambaye imemsainisha mkataba wa miaka miwili wenye kipangele cha kuongeza mwaka mmoja zaidi.