Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kisa cha Vinicius Jr, Benfica yaonja ‘Joto la Jiwe’

BENFICA Pict

Muktasari:

  • Benfica wanakabiliwa na faini kubwa pamoja na kuwekwa katika uangalizi maalum wa kufungiwa uwanja wao ikiwa mashabiki watafanya kosa kama hilo.

LISBON, URENO: Benfica imepigwa rungu na shirikisho la soka barani Ulaya UEFA kufuatia tabia ya kibaguzi ya mashabiki wao dhidi ya staa wa Real Madrid Vinicius Junior wakati wa mechi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Benfica wanakabiliwa na faini kubwa pamoja na kuwekwa katika uangalizi maalum wa kufungiwa uwanja wao ikiwa mashabiki watafanya kosa kama hilo.

Mbali ya adhabu ya UEFA Benfica yenyewe imechukua hatua za ndani kwa kuwasimamisha baadhi ya wanachama waliohusika na vitendo hivyo visivyokubalika.

UEFA ilitangaza Jumanne kuwa Benfica imepewa adhabu kali ambapo katika taarifa ya Kamati ya Usimamizi wa Maadili na Nidhamu ilieleza kuwa kulikuwa na vitendo vya ubaguzi.

Kutokana na hilo Benfica wametakiwa kupunguza idadi ya mashabiki 500 katika mechi yao ijayo ya Ligi ya Mabingwa Ulaya lakini adhabu hiyo itasubiri kwa kipindi cha mwaka mmoja ambapo itatazamwa na ikiwa kosa hilo litajirudia ndipo adhabu hiyo itaanza kufanya kazi. Pia Benfica imepigwa faini ya Euro 40,000 kwa matukio hayo ya ubaguzi.

Mbali na hilo UEFA pia imeitoza Benfica faini ya Euro 8,000 kwa matumizi ya taa za laser na Euro 25,000 kwa kurusha vitu uwanjani.

Hatua za kinidhamu pia zimelifikia benchi la ufundi la klabu hiyo ambapo kocha msaidizi Pedro Luis Ferreira Machado amefungiwa mechi moja ya mashindano ya UEFA kutokana na mwenendo usio wa kiungwana wakati wa mchezo huo uliokuwa na presha kubwa. Kwa jumla faini ya kifedha kwa matukio yote imefikia Euro 73,000.

Licha ya adhabu hizo kali kutoka UEFA Benfica imepongezwa kwa hatua yao ya haraka ya kutoa adhabu za ndani kwa wahusika.

Kwa mujibu wa gazeti la A Bola klabu hiyo iliwatambua mara moja wahusika wa vitendo hivyo na kuwapa adhabu.