Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Estevao Willian amfunika Vinicius Junior sokoni

Muktasari:

  • Hata hivyo pamoja na ukubwa wa jina lake, amejikuta akizidiwa kete na nyota wa Chelsea, Estevao katika chati ya wachezaji kutoka Brazil wenye thamani kubwa zaidi duniani kwa sasa.

LONDON, ENGLAND: VINICIUS Junior hapana shaka ndiye mchezaji wa Brazil ambaye jina lake linaimbwa katika maeneo mengi duniani kutokana na kiwango bora anachoonyesha katika kikosi cha Real Madrid.

Hata hivyo pamoja na ukubwa wa jina lake, amejikuta akizidiwa kete na nyota wa Chelsea, Estevao katika chati ya wachezaji kutoka Brazil wenye thamani kubwa zaidi duniani kwa sasa.

Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na taasisi ya CIES Football, thamani ya Estevao kwa sasa ni Pauni 102 milioni  ambayo ni mara tatu zaidi ya kiasi ambacho Chelsea walikitumia kumnunua.

Estevao ameonekana kupata wakati mgumu kuzoea maisha ya England tangu alipojiunga na Chelsea, Julai 14 mwaka jana akitokea Palmeiras ya kwao Brazil.

Hata hivyo mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 18, hadi sasa ameifungia Chelsea mabao mawili katika Ligi Kuu England, mabao matatu katika Ligi ya Mabingwa Ulaya na bao moja amepachika katika mashindano mengine ya ndani England.

Katika chati hiyo, mchezaji anayeshika nafasi ya pili kwa thamani kubwa ni nyota Joao Pedro ambaye anacheza sambamba na Estevao katika kikosi cha Chelsea.

Chelsea ilitumia kiasi cha Pauni 60 milioni kumnasa Pedro katika dirisha kubwa la usajili la majira ya kiangazi mwaka jana na kwa sasa ana thamani ya Pauni 98 milioni kwa mujibu wa utafiti huo wa CIES Football.

Pedro ameonekana kuwa katika kiwango bora cha kufumania nyavu katika siku za hivi karibuni na kuthibitisha hilo, mchezaji huyo katika mechi 29 za Ligi Kuu England msimu huu, ameifungia Chelsea mabao 14.

Vinicius Junior anashika nafasi ya tatu katika orodha ya wachezaji wa Kibrazil wenye thamani kubwa duniani hivi sasa akiwa na thamani ya Pauni 78 milioni.

Mchezaji anayeshika nafasi ya nne katika orodha hiyo ni Endrick Felipe anayechezea Olympique Lyon ambapo ana thamani ya Pauni 69 milioni na Savio wa Manchester City anashika nafasi ya tano akiwa na thamani ya Pauni 67 milioni.

Nyota wawili wa Arsenal, Gabriel Martinelli na Gabriel Magalhaes nao wapo katika chati hiyo ya wachezaji 10 wa Brazil wenye thamani kubwa zaidi duniani hivi sasa.

Martinelli yuko nafasi ya saba akiwa na thamani ya Pauni 60 milioni  na Magalhaes anashika nafasi ya 10 akiwa na thamani ya Pauni 47 milioni.