Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kigogo Man United azomewa Old Trafford

KIGO 01

Muktasari:

  • Bilionea huyo mwenye umri wa miaka 73 yuko chini ya shinikizo kubwa United kutokana na maamuzi kadhaa yenye utata tangu ainunue timu hiyo na kuwa msimamizi mkuu wa masuala ya michezo kuanzia mwaka 2024.

MANCHESTER, ENGLAND: BOSI wa Manchester United, Sir Jim Ratcliffe alizomewa na mashabiki alipowasili Old Trafford kwa ajili ya kutazama  dabi ya Manchester.

Bilionea huyo mwenye umri wa miaka 73 yuko chini ya shinikizo kubwa United kutokana na maamuzi kadhaa yenye utata tangu ainunue timu hiyo na kuwa msimamizi mkuu wa masuala ya michezo kuanzia mwaka 2024.

Klabu hiyo imefanya mabadiliko mengi katika miaka ya karibuni na wiki kadhaa zilizopita iliamua kumfuta kazi Kocha Ruben Amorim baada ya miezi 14 tu tangu aanze kuifundisha timu hiyo baada ya mwenendo mbaya wa matokeo.

Ratcliffe pia aliwahi kutupiwa sana lawama kwa kitendo chake cha kumwajiri na baadaye kumfuta mkurugenzi wa michezo Dan Ashworth ambaye alionekana kuipeleka timu katika mwelekeo sahihi.

SunSport imeeleza mashabiki kadhaa walimzomea Ratcliffe alipokuwa akiingia uwanjani kwa ajili ya mechi dhidi ya Manchester City.

KIGOGO Pict

Tajiri huyo alionekana kuwa mwenye tahadhari kubwa, akiwa ameinamisha kichwa huku amevaa koti la kijani lenye kofia juu ya kichwa chake.

Hata hivyo, hii siyo mara ya kwanza kwa mdosi huyo kuzomewa au kukumbana na upinzani kutoka kwa mashabiki wa mashetani hao wekundu.

Mapema Januari hii, kundi la mashabiki la Man United linaloitwa The 1958 walitangaza wataandamana mwezi ujao.

Kundi hilo lilitaka kupigwa kura ya kutokuwa na imani kwa wamiliki wote wa Man United na kusisitiza watafanya maandamano kabla ya mechi yao ya nyumbani dhidi ya Fulham Februari 1.

KIGO 02

Katika taarifa yao wamesema: “Baada ya kuyumba kwa klabu, Ratcliffe anaonekana kama kichekesho kisicho na uwezo. Badala ya klabu kuwa bora kila siku tumekuwa kichekesho kwa watu. Kipindi chake kimekuwa ni cha ajabu na kinachotia wasiwasi. Uwanjani, timu inacheza kwa kiwango cha chini, haina utambulisho mwelekeo wala malengo.  Nje ya uwanja, mambo ni mabaya zaidi."

Ratcliffe pia amekosolewa kwa kuongeza bei za tiketi, kuondoa punguzo la baadhi ya bidhaa kwa makundi maalum na kumwondoa Sir Alex Ferguson katika nafasi yake ya balozi.

Hata hivyo, katika mechi hiyo dhidi ya Man City, Man United ilishinda mabao 2-0 ikiwa ni ushindi wao mkubwa zaidi mbele ya majirani zao hao tangu mwaka 2021.