Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

KIBURI: Kevin Durant azidi kuitega Warriors

MATEREKA JALILU, DODOMA. WIKI iliyopita katika huu ukurasa wetu pendwa ilikuwepo habari inayomhusu staa Kevin Durant wa Golden State Warriors ambaye aliingizwa ndani ya uwanja mpya wa timu hiyo unaojengwa katika sehemu ya kuchezea tofauti na wachezaji wengine waliowahi kutembelea uwanja huo kutoruhusiwa kuingia sehemu ya kuchezea.

Katika habari ile tuliweka hisia za jinsi kuingizwa kwake ndani ya uwanja kulivyokuwa na maana kwa mabosi wa timu hiyo, hatua hiyo ilikuwa na lengo la kumfanya nyota huo atamani kubakia kikosini hapo ili awe sehemu ya wachezaji watakaoutumia uwanja huo mpya msimu ujao.

Sasa achana na hisia hizo, ishu mpya kumhusu Durant ni licha ya kupelekwa uwanjani hapo bado sio sababu za staa huyo anaweza kuondoka mwishoni mwa msimu huu baada ya rabsha iliyotokea kati yake na mchezaji mwenzake wa timu hiyo Draymond Green wiki hii.

Durant na Green waliibua rabsha katika mchezo wa kichapo cha timu yao dhidi ya Los Angeles Clippers na sio mara ya kwanza kwa nyota hao kupishana jambo ambalo linawaweka mtegoni mabosi wa timu hiyo kumbakiza mwishoni mwa msimu huu mkataba wake utakapomalizika.