Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kama huna hela, tiketi Kombe la Dunia 2026 hugusi

TIKETI Pict

Muktasari:

  • Kundi la mashabiki wa soka wa Ulaya limeibua mjadala na kufichua juu ya kushtushwa na kitendo cha Fifa kuweka kiingilio cha juu kwenye fainali hizo za Kombe la Dunia zitakazofanyika Marekani, Canada na Mexico na kutaka uuzwaji wa tiketi usitishwe haraka. Chama cha mashabiki wa soka wa England walibainisha kwamba bei ya tiketi za mechi za Kombe la Dunia 2026 haina tofauti na kupigwa kofi la usoni.

CALIFORNIA, MAREKANI: MASHABIKI wa soka wanaojiandaa kwenda kwenye fainali za Kombe la Dunia 2026 watakabiliwa na kasheshe zito la kuhusu bei ya tiketi za mechi kutokana na kuuzwa ghali sana.

Kundi la mashabiki wa soka wa Ulaya limeibua mjadala na kufichua juu ya kushtushwa na kitendo cha Fifa kuweka kiingilio cha juu kwenye fainali hizo za Kombe la Dunia zitakazofanyika Marekani, Canada na Mexico na kutaka uuzwaji wa tiketi usitishwe haraka. Chama cha mashabiki wa soka wa England walibainisha kwamba bei ya tiketi za mechi za Kombe la Dunia 2026 haina tofauti na kupigwa kofi la usoni.

Fifa bado haijasema kitu juu ya uamuzi huo wa upangaji wa bei za tiketi za fainali za Kombe la Dunia 2026.

Kwa mujibu wa BBC Sport ni kwamba inatambua tiketi za mchezo wa fainali utakaofanyika MetLife, New York, zimepangwa katika makundi matatu; Supporter value tier - Dola 4,185, Supporter standard tier - Dola 5,560 na Supporter premium tier - Dola 8,860 sawa na pesa za Kitanzania Sh10,256,514, Sh13,626,337 na Sh 21,713,911 mtawalia.

TIKE 02

Bei ya tiketi kwenye mechi hiyo ya fainali kwa Kombe la Dunia 2026 imezidi mara saba ya bei ya iliyokuwa ikiuzwa kwenye Kombe la Dunia 2022 huko Qatar, ambapo tiketi ya gharama ndogo katika fainali yenyewe iliuzwa kwa Pauni 450 sawa na Sh1,476,522 za Kitanzania.

Na haijaelezwa wazi juu ya tiketi kwa ajili ya mashabiki watoto na makundi maalumu. Na kwenye fainali hizo za Marekani, bei ya tiketi katika hatua ya makundi zimetofautiana kutokana na timu husika. Kwa mfano mashabiki wa England watalipa pesa nyingi kuangalia timu yao ukinganisha na mashabiki wa Scotland.

Kwenye fainali za Qatar miaka minne iliyopita, bei ya tiketi katika hatua ya makundi ilikuwa Pauni 68.50, Pauni 164.50 na Pauni 219. Lakini, sasa katika fainali hizo za Amerika, kwa mfano England, mechi yake dhidi ya Croatia itakayopigwa Juni 17, tiketi zake ni Pauni 198, Pauni 373 na Pauni 523. Kwenye mechi yao dhidi ya Ghana, tiketi ni Pauni 164, Pauni 320 na Pauni 447, huku mechi dhidi ya Panama tiketi ni Pauni 164, Pauni 346 na Pauni 462.

Kwa upande wa Scotland, bei ya tiketi kwa mechi zao mbili za kwanza kwenye hatua ya makundi ipo chini kulinganisha na England. Kwa mfano kwenye mechi dhidi ya Haiti tiketi zitakuwa Pauni 134, Pauni 298 na Pauni 372, wakati dhidi ya Morocco tiketi ni Pauni 163, Pauni 320 na Pauni 447. Lakini, kwenye mechi yao ya mwisho ya hatua ya makundi, ambapo watakipiga na Brazil, tiketi ya mechi yao itakuwa bei sawa na ile mechi ya England na Croatia.

TIKE 01

Kwa mechi za hatua ya robo fainali timu zote mechi zake tiketi zitakuwa za Pauni 507, Pauni 757 na Pauni 1,073, wakati kwenye nusu fainali tiketi zitakuwa za Pauni 686, Pauni 1,819 na Pauni 2,363.

Kwa mechi zote kwenye fainali hizo, mtu mmoja itamgharimu Pauni 5,225 kwa tiketi za chini, Pauni 8,580 kwa tiketi za kati na Pauni 12,357 kwa tiketi za daraja la juu. Kwenye fainali za Kombe la Dunia 2022, mtu mmoja kwa mechi zote aligharimikia Pauni 1,466, Pauni 2,645 na Pauni 3,914 kulingana na madaraja ya tiketi kuanzia kiingilio cha chini, kati na juu.