Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Jonathan David achanganya vigogo Ulaya

TETESI Pict

Muktasari:

  • David ambaye msimu huu amecheza mechi 41 za michuano yote na kufunga mabao 23 amezivutia timu nyingi kwa sababu mkataba wake unamalizika mwisho wa msimu huu, hivyo atakuwa anapatikana kama mchezaji huru.

NEWCASTLE imeungana na Manchester United, Tottenham, West Ham, Chelsea na Liverpool katika vita ya kuiwania saini ya mshambuliaji wa Lille na timu ya taifa ya Canada, Jonathan David, 25, katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi.

David ambaye msimu huu amecheza mechi 41 za michuano yote na kufunga mabao 23 amezivutia timu nyingi kwa sababu mkataba wake unamalizika mwisho wa msimu huu, hivyo atakuwa anapatikana kama mchezaji huru.

Mbali ya uwezo wake mkubwa wa kufunga, staa huyu pia ana uwezo mkubwa wa kusaidia timu kwa kutoa asisti ambapo msimu ameshatoa 10.

Fundi huyu pia anahitajika na baadhi ya timu za nje kama Hispania ikiwemo Barcelona ambayo imevutiwa naye.

Kutakiwa na klabu nyingi kunaweza pia kuongeza ugumu wa kumpata kwa ushindani wa ofa bora zaidi.


Hugo Ekitike

LIVERRPOOL imepanga kupambana na Arsenal kwa ajili ya saini ya mshambuliaji wa Frankfurt na timu ya taifa ya Ufaransa, Hugo Ekitike, 22, katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi.

Ekitike ambaye msimu huu ni miongoni mwa wachezaji tegemeo katika kikosi cha kwanza cha timu yake, amecheza mechi 38 za michuano yote na kufunga mabao 19. Pia anawindwa na Manchester United na Newcastle.


 Jarell Quansah

BEKI wa Liverpool ambaye ni raia wa England, Jarell Quansah, ameivutia Newcastle, inayojipanga kumsajili katika dirisha la majira ya kiangazi mwisho wa msimu, lakini changamoto kubwa inadaiwa kuwa Liverpool hawataki kumuuza kwa sasa.

Kocha wa Majogoo hao wa Jiji la Liverpool, Arne Slot bado ana imani kubwa na staa huyo na anaamini anaweza kuwa tegemeo kwa msimu ujao.

nje


Jeremie Frimpong

MANCHESTER City wanapanga kuanzisha tena mazungumzo kwa kwa ajili ya kumsaini beki wa kulia wa Bayer Leverkusen na timu ya taifa ya Uholanzi, Jeremie Frimpong, 24, katika dirisha lijalo.

Mbali ya Man City staa huyu pia anawindwa na Liverpool ambayo inataka kumsajili katika dirisha lijalo. Mkataba wa Frimpong unatarajiwa kumalizika mwaka 2028.


Darwin Nunez

LIVERPOOL wanatarajia kupokea ofa kubwa kutoka timu za Ligi Kuu ya Saudi Arabia kwa ajili ya kumuuza mshambuliaji wao na timu ya taifa ya Uruguay, Darwin Nunez, 25, katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi.

Nunez anahusishwa kuondoka kwa sababu kocha Arne Slot haridhishwi na kiwango chake alichoonyesha kwa msimu huu.


Cristian Romero

TOTTENHAM Hotspur imekataa kumuuza beki wake wa kimataifa wa  Argentina, Cristian Romero, 26, baada ya Atletico Madrid kuonyesha nia ya kutaka kumnunua katika dirisha lijalo.

Inaelezwa vigogo wa Atletico wanamtumia hadi Julien Alvarez kama sehemu ya ushawishi ya kumpata Romero. Mkataba wa staa huyu unatarajiwa kumalizika mwaka 2027.


Mathys Tel

BAYERN Munich inaangalia uwezekano wa kumrudisha mshambuliaji wake anayecheza kwa mkopo Tottenham, Mathys Tel, 19, katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi. Mabosi wa Bayern wanataka kuwarudisha mastaa hao akiwamo Tel kwa ajili ya kuwatumia katika michuano ya Kombe la Dunia la klabu. Mkataba wa Tel na Spurs unatarajiwa kumalizika 2029.


Francisco Trincao

MANCHESTER United, Newcastle na Arsenal zinapewa nafasi kubwa ya kumsajili winga wa Sporting Lisbon na Ureno, Francisco Trincao, 25, katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi.

Awali, ilionekana kuwa fundi huyu anaweza kwenda Barcelona kutokana na kipengele cha mkataba wa mauziano uliosainiwa kati ya Barca na Sporting wakati fundi huyu anauzwa. Ni zao la Barca.