Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Jesus pigo jipya Arsenal akipata majeraha

Jesus Pict

Muktasari:

  • Mchezaji huyo aliumia wakati akijaribu kuokoa shuti la Bruno Fernandes katika eneo la hatari la Arsenal na kujikuta akipata majeraha hayo ambayo huenda yakamuongeza katika orodha ya wachezaji wa timu ambao ni majeruhi.

LONDON, ENGLAND: Mkosi wa majeraha umeendelea kuiandama Arsenal kufuatia mshambuliaji wake Gabriel Jesus kuumia katika mchezo wa Kombe la FA, nyumbani dhidi ya Manchester United.

Mchezaji huyo aliumia wakati akijaribu kuokoa shuti la Bruno Fernandes katika eneo la hatari la Arsenal na kujikuta akipata majeraha hayo ambayo huenda yakamuongeza katika orodha ya wachezaji wa timu ambao ni majeruhi.

Jesus amepata maumivu hayo katika kipindi ambacho Arsenal inawakosa Bukayo Saka, Ethan Nwaneri, Ben White, Takehiro Tomiyasu na Riccardo Calafiori ambao wote ni majeruhi.

Majeraha hayo yalipelekea Jesus kufanyiwa mabadiliko katika dakika ya 40 kumpisha Raheem Sterling na kwa sasa inasubiriwa ripoti ya timu hiyo juu ya ukubwa wa majeraha ya mshambuliaji huyo.

Kama majeraha hayo yatakuwa makubwa, hapana shaka yanaweza kuilazimisha Arsenal kuingia sokoni kwa ajili ya kusaka mshambuliaji mpya katika kipindi hiki cha dirisha dogo la usajili.

Mchezaji huyo amekuwa akikabiliwa na majeraha ya mara kwa mara ambayo yamekuwa yakimfanya akose idadi kubwa ya mechi za timu hiyo katika mashindano tofauti.

Msimu huu, mshambuliaji huyo alikosa mechi mbili za mwanzo za msimu kutokana na majeraha ya goti ambayo aliyapata wakati wa maandalizi ya msimu.

Katika mechi za hivi karibuni, Jesus amekuwa msaada mkubwa katika safu ya ushambuliaji ya Arsenal kutokana na mabao ambayo ameyafunga ambapo kabla ya mechi ya jana, nyota huyo wa Brazil alifunga mabao matano katika mechi sita.

Jesus alijiunga na Arsenal mwaka 2022 akitokea Manchester City na kuanzia hapo hadi sasa, amecheza idadi ya mechi 95, akifunga mabao 26 na kupiga pasi 17 za mwisho.