Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Jack Grealish avamia jezi ya Rooney

JACK Pict

Muktasari:

  • Grealish, 29, amejiunga kwa mkopo wenye kipengele cha kusajiliwa jumla kwa dau la Pauni 50 milioni wakati wa dirisha lijalo la majira ya kiangazi na amekabidhiwa jezi iliyovaliwa na magwiji kibao wa miamba hiyo.

LIVERPOOL, ENGLAND: JACK Grealish hatimaye amefanikiwa kukimbia benchi huko Manchester City baada ya kusajili mkataba wa mkopo wa msimu mmoja huko Everton.

Grealish, 29, amejiunga kwa mkopo wenye kipengele cha kusajiliwa jumla kwa dau la Pauni 50 milioni wakati wa dirisha lijalo la majira ya kiangazi na amekabidhiwa jezi iliyovaliwa na magwiji kibao wa miamba hiyo.

Grealish atavaa jezi Namba 18 kwenye klabu hiyo, akipita kwenye nyayo za magwiji wa Everton, Paul Gascoigne na Wayne Rooney, ambao walitinga jezi zenye namba hiyo mgongoni wakati walipokuwa wakikipiga mahali hapo.

Akizungumzia kuchagua namba hiyo, Grealish alisema: “Kuna sababu ya kuchagua Namba 18. Kuna namna nyingine, lakini wachezaji wawili wa Kiingereza niwapendao, Wayne Rooney na Paul Gascoigne, wote walivaa Namba 18. Punde nilipofahamu dili linakaribia kutiki, nilitazama na kuona Namba 18 ipo wazi, hivyo niliona hiyo ni sahihi kwangu na nikaanzia hapo.

“Nilizungumza na Wayne (Rooney) kabla sijaja hapa na nilimwambia kuhusu Namba 18, naye alifurahia!”

Mwezi uliopita Grealish aliripotiwa kukubali kufanya mazoezi kivyake tofauti na wachezaji wenzake wa Man City jambo lililotia shaka kubwa kuhusu hatima ya maisha yake huko Etihad.

Kocha Pep Guardiola alimweka kando pia staa huyo wa zamani wa Aston Villa kwenye kikosi chake kilichokwenda kwenye Kombe la Dunia la Klabu huko Marekani. Winga huyo alianzishwa kwenye mechi saba tu za Ligi Kuu England msimu uliopita. Na sasa staa huyo atakwenda kuwa chini ya kocha David Moyes huko Merseyside.

Akizungumzia uhamisho wake, Grealish alisema: “Najiona kama nipo mwezini baada ya kusaini Everton. Ni jambo kubwa kwangu, kusema ukweli. Hii ni klabu kubwa na yenye mashabiki makini. Baada ya kuzungumza na kocha, nilifahamu hapo ni mahali pekee ninapohitaji kwenda.”