Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ibrahima Konate aingia anga za PSG

TETESI Pict

Muktasari:

  • Licha ya muda wa mkataba wake kuwa ni mchache, hadi sasa Konate bado hajafikia makubaliano yoyote na vigogo wa Liverpool juu ya kuurefusha.

PARIS St-Germain na Real Madrid wanafuatilia hali ya beki wa Liverpool na Ufaransa, Ibrahima Konate, 25, ili kumsajili katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi ambapo mkataba wake utakuwa umebakisha mwaka mmoja kabla ya kumalizika.

Licha ya muda wa mkataba wake kuwa ni mchache, hadi sasa Konate bado hajafikia makubaliano yoyote na vigogo wa Liverpool juu ya kuurefusha.

Konate ambaye msimu huu amecheza mechi 34 za michuano yote, akifunga mabao mawili na kutoa asisti mbili anadaiwa kuwa alifanya mazungumzo na mabosi wa PSG katika mchezo wao wa mwisho wa Ligi ya Mabingwa hatua ya 16 bora uliopigwa Anfield.

Ingawa mkataba wake haujabakisha muda mrefu hadi kuisha, Liverpool haionekani kuwa tayari kumuuza staa huyu na ikitokea kumuuza huenda ikahitaji kiasi kikubwa cha pesa ili kufanya hivyo.


Douglas Luiz

NOTTINGHAM Forest imepanga kurudi mezani na kuzungumza na Juventus ili kuipata saini ya kiungo Douglas Luiz, 26, katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi.

Awali, Nottingham Forest ilijaribu kutuma ofa kwenda Juventus katika dirisha la majira ya baridi mwaka huu lakini ilishindikana kufikia mwafaka. Mkataba wa sasa wa Mbrazili huyu aliyewahi kutamba EPL unatarajiwa kumalizika mwaka 2029.


Jarrad Branthwaite

EVERTON inataka kumsajili beki wa kati wa Genoa, Koni de Winter, 22, kama mbadala wa beki wao raia wa England, Jarrad Branthwaite, 22, ambaye anahusishwa kuondoka mwisho wa msimu huu.

Branthwaite amekuwa akihusishwa na vigogo wengi wa Engand ambao wanahitaji kumsajili mwisho wa msimu huu ili kuboresha safu zao za ulinzi akizivutia kutokana na ubora wake na umri wake kuwa mdogo.


Luis Diaz

MSHAMBULIAJI wa Liverpool na Colombia, Luis Diaz, 28, amewaambia wawakilishi wake kwamba anahitaji kutua Barcelona katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi. Diaz ambaye ni miongoni mwa mastaa tegemeo wa Liverpool moja kati ya ndoto yake kubwa ni kuichezea Barca na wakati huu ambapo mkataba wake unaelekea ukingoni anaona ni muda sahihi.


Kepa Arrizabalaga

Bournemouth ipo kwenye mchakato wa kuwasilisha ofa ili kumsainisha mkataba wa kudumu kipa wa Chelsea na timu ya taifa ya Hispania, Kepa Arrizabalaga, 30, ambaye msimu huu anaicheza kwa mkopo. Mabosi wa Bournemouth wamevutiwa sana na kiwango cha Kepa alichokionyesha tangu ajiunge nao. Chelsea ipo tayari kumwachia kwani hayupo katika mipango ya kocha Enzo Maresca.


Lamare Bogarde

SEVILLA inajipanga kutuma ofa kwenda Aston Villa ili kuipata huduma ya kiungo wa timu hiyo  mwenye umri wa miaka 21, Lamare Bogarde, mwisho wa msimu huu.

Bogarde pia ameonyesha nia ya kuwa tayari kuondoka ili kupata nafasi kubwa zaidi ya kucheza tofauti na ilivyo sasa. Msimu huu amecheza mechi 18 za michuano yote.


Johan Martinez

BAYER Leverkusen, Parma na Wolfsburg zimejumuika na Liverpool, Manchester City na Brighton katika vita ya kuiwania saini ya kiungo wa Independiente del Valle raia wa Ecuador, Johan Martinez, 15, katika dirisha lijalo. Maskauti wa timu hizi wanadaiwa kutembelea Ecuador kwa ajili ya kumtazama Martinez ambaye ni mmoja kati ya makinda wenye vipaji.


Rayan Cherki

OLYMPIQUE Lyon ipo tayari kumuuza winga wake wa kimataifa wa Ufaransa, Rayan Cherki, 21,  mwishoni mwa msimu ambapo vigogo mbalimbali ikiwamo Liverpool, Bayern Munich na Borussia Dortmund  zimeonyesha nia ya kutaka kumsajili. Cherki amevutia vigogo hawa tangu mwaka jana kutokana na ubora wake aliouonyesha tangu msimu uliopita.