Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Huyo Cristiano Ronaldo ni mabao tu

RONALDO Pict

Muktasari:

  • Bao lake alilofunga kwenye fainali ya Kombe la Saudi Arabia akiwa na kikosi cha Al Nassr dhidi ya Al-Ahli lililiwa la 100 tangu alipotua huko Mashariki ya Kati.

RIYADH, SAUDI ARABIA: SUPASTAA, Cristiano Ronaldo amekuwa mchezaji wa kwanza kwenye historia ya soka kufunga mabao 100 au zaidi katika klabu nne tofauti, lakini bado ameshindwa kuisaidia timu yake kubeba taji la Saudi Super Cup.

Bao lake alilofunga kwenye fainali ya Kombe la Saudi Arabia akiwa na kikosi cha Al Nassr dhidi ya Al-Ahli lililiwa la 100 tangu alipotua huko Mashariki ya Kati.

Sasa mkali huyo wa Ureno mwenye umri wa miaka 40, amefikisha idadi kama hiyo ya mabao na zaidi katika timu za Real Madrid, Ureno, Manchester United na Juventus. Bao lake alifunga kwa mkwaju wa penalti kuifanya Al Nassr kuongoza 1-0. Hata hivyo, fursa ya kubeba taji la kwanza kubwa huko Al-Nassr ilizimwa na Al-Ahli iliyoshinda kwa mikwaju ya penalti baada ya sare 2-2.

Ronaldo alifunga mkwaju wake wa penalti, lakini aliangushwa na wenzake wakati Ahli iliposhinda kwa penalti 5-3.

Ronaldo alifunga kwa penalti, lakini Frank Kessie alisawazisha, kisha Marcelo Brozovic kuja kuifanya Al-Nassr kuongoza tena kabla ya Roger Ibanez kusawazisha na kufanya mechi hiyo kuingia kwenye kupigiana penalti.

Ronaldo alikwenda wa kwanza kupiga mkwaju wa penalti na kufunga na kisha kutokana na wengine kufunga hadi hapo Abdullah Al-Khaibari alipokosa. Hilo lilimfanya staa wa zamani wa FC Porto, Galeno kupata nafasi ya kushinda.

Ronaldo anaendelea kufunga mabao akifukuzia rekodi ya kufikisha mabao 1000 kwenye maisha yake ya soka na sasa ameshafikisha 939.

Huko kwenye kikosi cha Al Nassr, Ronaldo amefunga mabao 100 katika mechi 107 na supastaa huyo wa Ureno bado hajamaliza kazi yake ya kufunga.