Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Hojlund asakwa Italia kisa Mbeumo

Muktasari:

  • Miamba hiyo ya soka ya Italia inasaka straika mpya na inaamini Man United itakuwa tayari kumpiga bei mshambuliaji wao huyo ambaye ameshindwa kuwasha moto.

MILAN, ITALIA: AC MILAN inapiga hesabu za kunasa saini ya straika Rasmus Hojlund baada ya Manchester United kufikia makubaliano ya kumsajili Bryan Mbeumo kutoka Brentford.

Miamba hiyo ya soka ya Italia inasaka straika mpya na inaamini Man United itakuwa tayari kumpiga bei mshambuliaji wao huyo ambaye ameshindwa kuwasha moto.

Man United ilimsajili Hojlund, 24, miaka miwili iliyopita kwa ada ya Pauni 72 milioni.

Lakini, hakuwa na msimu bora, wakati alipofunga mara nne tu kwenye Ligi Kuu England na Man United imeshusha bei yake, ikimuuza kwa Pauni 29.5 milioni tu.

Milan sasa inatafuta namna ya kwenda kukubaliana na Man United kwa ajili ya dili la mshambuliaji huyo. Mchezaji mwenyewe, Hojlund amebainisha dhamira yake ya kutaka kubaki Old Trafford ili kuonyesha thamani yake, wakati mkataba wake ukiisha 2028.

Lakini, kupata nafasi ya kucheza kwa msimu ujao inaweza kuwa ngumu baada ya Man United kukubali kulipa Pauni 71 milioni kunasa saini ya Mbeumo.

Mbeumo, 25, alifunga mabao 20 kwenye Ligi Kuu England msimu uliopita akiwa na kikosi cha Brentford.


Na katika mfumo wa kocha Ruben Amorim wa 3-4-3, Mbeumo anatarajia atakuwa upande wa kulia, huku staa mwingine mpya wa Man United, Matheus Cunha, aliyesajiliwa kwa Pauni 62.5 milioni kutoka Wolves atakuwa upande wa kushoto. Mbrazili huyo, Cunha, 26, alifunga mabao 15 na kuasisti sita kwenye Ligi Kuu England msimu uliopita.

Na kama Hojlund ataondoka na Man United itashindwa kusajili straika mwingine wa kati, basi eneo hilo la straika kwa msimu ujao anaweza kucheza mkali wa Uholanzi, Joshua Zirkzee.