Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Hebu msikieni kocha Arne Slot

SLOT Pict

Muktasari:

  • Liverpool imetumia mkwanja mrefu karibu Pauni 300 milioni kusajili na bado inaweza kutumia pesa ndefu zaidi. Lakini, mabingwa hao watetezi wameingiza karibu Pauni 150 milioni kwenye mauzo ya wachezaji dirisha hili.

LIVERPOOL, ENGLAND: KOCHA wa Liverpool, Arne Slot amesema timu hiyo inaweza kupewa nafasi kubwa ya kubeba taji la Ligi Kuu England msimu huu, lakini hilo si kwa sababu ya pesa ambazo wametumia kusajili kwenye dirisha hili.

Liverpool imetumia mkwanja mrefu karibu Pauni 300 milioni kusajili na bado inaweza kutumia pesa ndefu zaidi. Lakini, mabingwa hao watetezi wameingiza karibu Pauni 150 milioni kwenye mauzo ya wachezaji dirisha hili.

Slot alisema: “Kama ulishinda msimu uliopita ni kawaida kupewa nafasi kubwa ya kushinda tena msimu unaofuata. Kwangu mimi haiwezi kuwa hivyo kama tunazungumzia matumizi, kwa sababu sisi hatukutumia pesa nyingi sana kulinganisha na wengine. Lakini, ukiniambia tunapewa nafasi kubwa kwa sababu tulishinda msimu uliopita, hilo naelewa. Wachezaji, tumesajili wazuri kama ambavyo timu nyingine zilivyofanya pia.”

Liverpool ilitumia Pauni 10 milioni tu msimu uliopita kumsajili Federico Chiesa kisha ilivuna pesa nyingi kwa wale walioondoka.

Dirisha hili imevunja rekodi ya uhamisho Uingereza kwa kutumia Pauni 116 milioni kumsajili Florian Wirtz, huku imeweka mezani Pauni 120 milioni pia ikimtaka Alexander Isak.

Arsenal imetumia karibu Pauni 200 milioni kwenye dirisha hili la majira ya kiangazi, huku yenyewe ikiingiza Pauni 9 milioni tu, wakati Manchester United ikimsajili Benjamin Sesko itafikisha matumizi ya Pauni 200 milioni na bado hajapata pesa yoyote iliyoingiza kwenye mauzo ya mastaa wake.

Manchester City imetumia Pauni 151 milioni kwenye dirisha hili, pia ilitumia pesa nyingi Januari, wakati yenyewe iliingiza Pauni 42 milioni.

Huku Chelsea pia imetumia zaidi ya Pauni 200 milioni, lakini imeingiza zaidi ya Pauni 100 milioni kwenye mauzo ya mastaa.