Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

He! Merino ataka aongezwe mshahara

MERINO Pict

Muktasari:

  • Kiungo huyo wa Kihispania amefunga mabao manne, likiwamo la ushindi kwenye mechi ya wikiendi iliyopita dhidi ya Chelsea kwenye Ligi Kuu England.

LONDON, ENGLAND: UMESIKIA hii? Staa mpya wa Arsenal, Mikel Merino anataka apandishiwe mshahara wake kutokana na sasa kufanya majukumu mengine kabisa tofauti na yaliyofanya asajiliwe.

Kiungo huyo wa Kihispania amefunga mabao manne, likiwamo la ushindi kwenye mechi ya wikiendi iliyopita dhidi ya Chelsea kwenye Ligi Kuu England.

Staa huyo kwa sasa anatumika na kocha Mikel Arteta kama Namba 9 bandia baada ya kikosi hicho cha Arsenal kutokuwa na straika yeyote wa asili kufuatia Kai Havertz na Gabriel Jesus kuwa majeruhi na hawataonekana uwanjani hadi msimu ujao.

Baada ya kushindwa kumsajili straika Ollie Watkins kwenye dirisha la Januari, Arsenal inatarajia kuingia sokoni kwenye dirisha lijalo kusaka straika mpya ili kumaliza tatizo.

Lakini, Merino alipoulizwa kama Arsenal haihitaji tena straika kutokana na mabao yake, kiungo huyo aliyesajiliwa kwa Pauni 27.4 milioni alisema: "Hilo swali ni la (Mikel) Arteta na mkurugenzi mpya wa michezo."

Na alipoulizwa kuhusu ujio wa bosi mpya wa michezo, Andrea Berta, ambaye alikuwa mkurugenzi wa michezo kwenye klabu ya Atletico Madrid, Merino alisema: "Andrea Berta? Sijui kama hiyo imeshakuwa rasmi, sijui chochote."

Baadaye, kiungo huyo Mhispaniola alitania, akisema: "Lakini, nitafanya kitu kimoja, nitamwomba anipe mkataba wa mshambuliaji, wanalipwa pesa nyingi na mimi nina majukumu mawili ndani ya uwanja."

Arsenal inatarajia kumpokea kikosini mshambuliaji wao Bukayo Saka kwenye mechi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya hatua ya robo fainali dhidi ya Real Madrid itakayopigwa Aprili 8. Na kiungo Merino, aliyenaswa kutoka Real Sociedad alisema: "Itakwenda kuwa mechi ngumu sana. Ni changamoto ya kihistoria kwetu na tuna njaa kwelikweli."