Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Hatua ya 16 bora Ligi ya Mabingwa Ulaya ni moto!

UEFA Pict

Muktasari:

  • Man City ya kocha Pep Guardiola ilisukumwa nje ya michuano hiyo na Real Madrid msimu uliopita. Droo hiyo ilifanyika mjini Nyon, Uswisi mchana wa Ijumaa na kuonyesha namna mtoano utakavyokuwa.

NYON, USWISI: NI kivumbi na jasho. Droo ya hatua ya mtoano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kwenye 16 bora imepangwa, huku ikiipa nafasi Manchester City kukutana na mabingwa wa Kihistoria, Real Madrid katika mechi iliyojaa visasi.

Man City ya kocha Pep Guardiola ilisukumwa nje ya michuano hiyo na Real Madrid msimu uliopita. Droo hiyo ilifanyika mjini Nyon, Uswisi mchana wa Ijumaa na kuonyesha namna mtoano utakavyokuwa.

Baada ya kukutana mara kadhaa katika misimu iliyopita, Guardiola atawakabili tena wapinzani wake wa zamani. Wakati huo huo, Chelsea imepangwa kukutana na mabingwa watetezi Paris Saint-Germain katika moja ya mechi inayotazamiwa kuwa na upinzani mkali. Mechi hiyo ya Chelsea na PSG ni kumbukumbu ya fainali ya Kombe la Dunia la Fifa, wakati The Blues iliposhinda 3-0, shukrani kwa mabao ya Cole Palmer, aliyefunga mara mbili na Joao Pedro. Liverpool itacheza dhidi ya klabu ya Uturuki, Galatasaray, yenye mastaa kibao akiwamo Victor Osimhen, huku Arsenal ikitarajiwa kuvaana na timu ya Ujerumani, Bayer Leverkusen.

Tottenham na Newcastle zimepangiwa wapinzani kutoka Hispania katika hatua ya 16 bora. Kikosi cha Eddie Howe kitamenyana na Barcelona, wakati Tottenham itakutana na Atletico Madrid.

Mechi za mkondo wa kwanza za hatua ya 16 bora zitachezwa Machi 10 na 11, huku mkondo wa marudiano ikipangwa kufanyika wiki inayofuata. Ingawa klabu sasa zinajua wapinzani wao wa 16 bora, pia vimefahamu uwezekano wa wapinzani wao katika hatua zinazofuata za mashindano, baada ya ratiba kamili ya mtoano kupangwa. Arsenal itakapopenya mbele ya Leverkusen itakabiliana na mshindi wa mechi baina ya kiboko ya vigogo Bodo/Glimt na Sporting Lisbon kwenye hatua ya robo fainali.

Man City na Real Madrid zikimalizana kwenye nafasi ya 16 bora, mshindi atakwenda kucheza na mshindi kati ya Bayern Munich au Atalanta kwenye robo fainali, huku hatua hiyo ikitarajia kushuhudia miamba miwili ya Ligi Kuu England.

Chelsea na Liverpool zitakutana kwenye nane bora endapo endapo kama itazitupa nje PSG na Galatasaray mtawalia. Newcastle itakipiga na Barcelona, ikiwa ni mechi ya kisasi pia na timu hizo zilikutana kwenye hatua ya ligi, Septemba mwaka jana na Marcus Rashford, alifunga mara mbili kuipa ushindi wa 2-1 Barcelona uwanjani St James’ Park.

Arsenal ilifuzu moja kwa moja hatua ya 16 bora baada ya kumaliza kileleni mwa msimamo wa hatua ya awali ya ligi kwa kushinda mechi zote nane. Timu nyingine za England zilizofuzu moja kwa moja hatua ya 16 bora ni pamoja na Liverpool, Tottenham, Chelsea na Man City, huku Newcastle United ililazimika kupitia kwenye mchujo na ililazimika kuisukuma nje Qarabag ili kukamatia tiketi hiyo ya 16 bora.

Fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya itafanyika uwanjani Puskas Arena mini Budapest, Mei 30.

RATIBA KAMILI YA 16 BORA YA LIGI YA MABINGWA

Real Madrid vs Man City

PSG vs Chelsea

Newcastle vs Barcelona

Bodo/Glimt vs Sporting Lisbon

Galatasaray vs Liverpool

Atletico vs Tottenham

Bayer Leverkusen vs Arsenal

Atalanta vs Bayern Munich