Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

16 bora Ligi ya Mabingwa Ulaya, Courtois anaitaka Man City 

UEFA Pict

Muktasari:

  • Courtois ameyasema hayo baada ya ushindi wa 2-1 ilioupata Real Madrid dhidi ya Benfica usiku wa jana Jumatano Februari 25, matokeo yaliyohakikisha Madrid kusonga mbele kwa jumla ya mabao 3-1.

KIPA wa Real Madrid, Thibaut Courtois, ametabiri kuwa kikosi chao kitakutana na Manchester City katika hatua ya 16 bora ya Ligi ya Mabingwa Ulayua, kupitia droo itakayofanyika kesho Ijumaa.

Courtois ameyasema hayo baada ya ushindi wa 2-1 ilioupata Real Madrid dhidi ya Benfica usiku wa jana Jumatano Februari 25, matokeo yaliyohakikisha Madrid kusonga mbele kwa jumla ya mabao 3-1.

Katika hatua inayofuata, Real Madrid itakabiliana na Manchester City au Sporting Lisbon.

“Wote tunajua itakuwa Man City kwenye droo ya Ijumaa. Wote wanajua hivyo.” Courtois amesema.

Real Madrid na Manchester City zilishakutana awali kwenye hatua ya makundi, ambapo timu ya kocha Pep Guardiola ilishinda 2-1 kwenye Uwanja wa Bernabeu. Ushindi huo unaleta matukio ya kuvutia zaidi wakati Real Madrid inajiandaa miamba hiyo ya England.

Hatua ya 16 bora ya Ligi ya Mabingwa Ulaya ni mzunguko muhimu wa mashindano ya klabu bora barani Ulaya, ambapo timu zinazofanya vizuri katika hatua ya makundi hukutana ili kuamua ni nani atakayosonga mbele hadi robo fainali.

Kila timu inayoshiriki katika hatua hii inakabiliana na mpinzani wake kwa mechi mbili, nyumbani na ugenini, ambapo jumla ya mabao ya mechi zote mbili huamua mshindi. Katika baadhi ya misimu, baadhi ya timu zinapita awali kupitia playoff ya knockout, ambayo huamua ni timu zipi zitashiriki hatua ya 16 bora.

Kwa mfano, katika msimu huu wa 2025-2026, baadhi ya timu kama Real Madrid na Manchester City zimeripotiwa kuingia hatua hii, huku ushindi wa jumla ukihesabiwa kutoka mechi za awali za playoff.

Ligi ya Mabingwa Ulaya inachukua nafasi muhimu kwa klabu hizi kwani ni hatua ya kwanza ya mtoano kamili, ikiwapa kila timu nafasi ya kuonyesha uwezo wake, wachezaji nyota, na mbinu za kiufundi zinazoamua ni nani atakayefuzu kwenye robo fainali na hatimaye kutwaa taji la Ulaya.

Tayari mashabiki wa soka barani Ulaya wanasubiri droo itakayofanyika kesho Ijumaa, Februari 27, 2026 ili kujua mechi zinazotarajiwa na wachezaji wanaohusiana na ushindani mkali katika jukwaa la Mabingwa Ulaya.

Nane zilizofuzu moja kwa moja

  1. Arsenal FC
  2. FC Bayern München
  3. Liverpool FC
  4. Tottenham Hotspur FC
  5. FC Barcelona
  6. Chelsea FC
  7. Sporting CP
  8. Manchester City FC


Nane zilizofuzu kwa tiketi ya mchujo

9. Real Madrid CF

10. FC Internazionale Milano

11. Paris Saint-Germain

12. Newcastle United FC

13. Juventus FC

14. Atlético Madrid

15. Atalanta BC

16. Bayer 04 Leverkusen