Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Haaland haogopi kesi ya Man City

Muktasari:

  • Haaland alisaini mkataba wa miaka tisa na nusu kwenye kikosi hicho cha Man City, Januari mwaka huu huku miamba hiyo ya Etihad ikisubiri hatima yao juu ya hukumu inayoweza kutokana na kesi hiyo inayowakabili juu ya masuala ya kipato ya matumizi.

MANCHESTER, ENGLAND: STRAIKA Erling Haaland amefichua mabosi wa Manchester City wamemhakikishia watashinda mashtaka yao 130 yanayowakabili dhidi ya Ligi Kuu England juu ya madai ya udanganyifu kwenye mapato na matumizi.

Haaland alisaini mkataba wa miaka tisa na nusu kwenye kikosi hicho cha Man City, Januari mwaka huu huku miamba hiyo ya Etihad ikisubiri hatima yao juu ya hukumu inayoweza kutokana na kesi hiyo inayowakabili juu ya masuala ya kipato ya matumizi.

Man City imekuwa ikisisitiza kwamba haina hatia kwenye jambo hilo, lakini kinachoelezwa ni endapo watakutwa na hatia basi adhabu inayoweza kuwakabili ni kupokwa pointi hadi 100.

Haaland ana uhakika hakuna kitu kibaya kitakachokwenda kuitokea Man City baada ya kusaini mkataba mpya, ambao unadaiwa kuwa na kipengele kinachoruhusu kuvunjwa ikitokea vinginevyo.

Alipozungumza baada ya kusaini dili hilo Januari mwaka huu, straika huyo wa mabao alisema: “Nina furaha kusaini mkataba mpya na kuendelea kubaki kwenye klabu hii. Man City ni klabu spesho, yenye watu makini na mashabiki sahihi kabisa wanaleta mazingira ya kila mtu kucheza kwa ubora mkubwa. Napenda pia kumshukuru Pep, benchi lake la ufundi na kila mtu ambaye amekuwa msaada kwangu kwa miaka hii.â€

Guardiola naye amekuwa na uhakika na klabu hiyo baada ya kusaini mkataba wa miaka miwili wa kuendelea kubaki na hakuwa na hofu ya timu kushushwa daraja endapo kama itakutwa na hatia kwenye mashtaka hayo 130.