Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Haaland aweka mzigo kwenye chesi

Muktasari:

  • Mshambuliaji huyo wa Manchester City ameafikiana kutoa ufadhili kwa mashindano yajulikanayo kama Total Chess World Championship Tour. Mradi huo unatarajiwa kumshirikisha bingwa namba moja duniani, Magnus Carlsen, ambaye pia ni raia wa Norway kama alivyo Haaland.

OSLO, NORWAY: STRAIKA supastaa wa kimataifa wa Norway, Erling Haaland, amekubali kuwekeza mamilioni katika mashindano mapya ya mchezo wa chesi yenye zawadi ya Pauni 2 milioni.

Mshambuliaji huyo wa Manchester City ameafikiana kutoa ufadhili kwa mashindano yajulikanayo kama Total Chess World Championship Tour. Mradi huo unatarajiwa kumshirikisha bingwa namba moja duniani, Magnus Carlsen, ambaye pia ni raia wa Norway kama alivyo Haaland.

Kwa mujibu wa The Guardian, Haaland amekubali kuwa mwekezaji saa chache tu kabla ya mechi ya mwisho ya Ligi Kuu England msimu huu. Hii ilikuwa kabla ya sare ya 1-1 dhidi ya West Ham United Jumamosi wiki iliyopita.

Nyota huyo alionekana akivaa kofia ya Norway Chess alipokuwa akiingia katika Uwanja wa London kabla ya mchezo kuanza, ambapo mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 ameungana na mfanyabiashara Morten Borge kuanzisha kampuni iitwayo Chess Mates.

Kundi lao litakuwa na umiliki mkubwa katika mashindano ya chesi ya Norway ndani ya Total Chess World Championship Tour. Baada ya uwekezaji huo, Haaland alisema: “Chesi ni mchezo wa ajabu sana. Unaongeza makali ya akili, na kuna mambo mengi yanayofanana na soka, unapaswa kufikiria haraka, kuamini hisia zako na kupanga hatua kadhaa mbele.”

Mashindano ya kwanza yanatarajiwa kufanyika baadaye mwaka huu, huku msimu kamili wa mashindano hayo ukitarajiwa kuanza 2027.

Haaland aliongeza: “Nawekeza katika mashindano ya chesi ya Norway kwa sababu naamini Total Chess World Championship Tour inaweza kuifanya chesi kuwa mchezo mkubwa zaidi kwa watazamaji duniani kote. Timu inayosimamia mashindano ya chesi ya Norway tayari imefanya kazi nzuri kukuza mashindano haya.”

Ushiriki wa Magnus Carlsen unatarajiwa kuwa muhimu kwa mafanikio ya mashindano hayo, ambaye alikuwa bingwa wa dunia kuanzia 2013 hadi 2023 na bado ni namba moja duniani.

Haaland siyo mchezaji wa kwanza wa Ligi Kuu England kuonyesha mapenzi yake kwenye chesi, kwani 2023 nyota wa Liverpool, Mohamed Salah, alikiri kuwa ‘ameathiriwa’ na mchezo huo. Wakati huohuo, Eberechi Eze aliwahi kushinda Pauni 15,000 baada ya kushinda mashindano ya watu mashuhuri mwezi Mei, mwaka huu. Kocha wa Manchester City, Pep Guardiola naye pia aliwahi kujihusisha na mchezo wa chesi hapo awali.