Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Haaland amvuta kipa Bounou Man City

Muktasari:

  • Man City ya kocha Pep Guardiola ilikipiga na miamba hiyo ya Saudi Pro League katika mechi ya funga nikufunge na kushuhudia Al-Hilal ikisonga mbele kwa ushindi wa mabao 4-3 katika mchezo wa hatua ya mtoano ya raundi ya 16 bora.

FLORIDA, MAREKANI: STRAIKA Erling Haaland ameonekana kumshawishi kijanja kipa Yassine Bounou ajiunge Manchester City baada ya kuisaidia Al-Hilal kuiondoa miamba hiyo ya Ligi Kuu England fainali za Kombe la Dunia la Klabu na kutinga robo fainali.

Man City ya kocha Pep Guardiola ilikipiga na miamba hiyo ya Saudi Pro League katika mechi ya funga nikufunge na kushuhudia Al-Hilal ikisonga mbele kwa ushindi wa mabao 4-3 katika mchezo wa hatua ya mtoano ya raundi ya 16 bora.

Al-Hilal ilitinga hatua ya robo fainali, shukrani kwa kiwango bora kabisa cha kipa Bounou, aliyewagomea Man City kwa mashambulizi kibao. Na kutokana na hilo, Haaland aliamua kumpa maua yake baada ya filimbi ya mwi-sho ya mchezo huo.

Na kilichokuwa kikionekana ni kama straika huyo wa Norway anampa ishara Bounou ‘njoo ujiunge kwetu’ wakati alipokuwa akitafakari kipigo hicho cha kushtua. Wakati Haaland akipambana na hilo, kipa namba moja wa Man City, Ederson alikuwa na siku mbaya kwenye mechi alipoonyesha kiwango cha hovyo. Lakini, kumekuwa na uvumi kwamba kipa huyo Mbrazili anaweza kuachana na Man City huku timu za Saudi Arabia zikihusishwa naye. Kipa huyo wa zamani wa Benfica anaingia mwaka wake wa mwisho wa mkataba huko Etihad, hata hivyo ameweka kando mpango wa kuondoka. “Hatima yangu ipo hapa,” alisema Ederson.

“Baadhi ya marafiki zangu wanatimua stori nyingi, lakini asilimia 99 ni za uongo. Nawaelewa waandishi, wanataka habari na vitu vya kuposti mitandaoni. Akili yangu ipo hapa. Nitabaki kwenye hili jiji. Nitajitolea kila kitu kwenye Ligi Kuu England na kujaribu kushinda Ligi ya Mabingwa Ulaya.”