Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ghafla Trossard amekuwa mwili jumba

TROSSAD Pict

Muktasari:

  • Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 31 alitua Arsenal akitokea Brighton wakati wa dirisha la Januari 2023, ilipolipwa ada ya Pauni 20 milioni na nyongeza ya Pauni 7 milioni.

LONDON, ENGLAND: MASHABIKI wa Arsenal wamebaki vinywa wazi kutokana na mabadiliko ya ajabu ya mwili wa Leandro Trossard katika kipindi cha miaka mitatu aliyokaa kwenye kikosi hicho cha Emirates.

Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 31 alitua Arsenal akitokea Brighton wakati wa dirisha la Januari 2023, ilipolipwa ada ya Pauni 20 milioni na nyongeza ya Pauni 7 milioni.

Kwa haraka Trossard alijitengenezea nafasi muhimu kwenye kikosi cha Arsenal, akifunga na kuasisti katika mechi mbalimbali kuipa nguvu timu yake ya kushindania mataji.

Na juhudi zake nje ya uwanja zimekuwa za kuvutia vilevile, kulingana na wenzake kwenye timu.

Katika mahojiano ya hivi karibuni na Sky Sports, beki wa kati wa Arsenal, Gabriel Magalhaes alimsifu Trossard kwa bidii yake mazoezini.

Gabriel alipoulizwa ni nani “mnyama zaidi gym,”, alimtaja Kai Havertz kabla ya kuongeza:

“Leandro Trossard. Ee Mungu wangu, huyu jamaa… Ana nguvu sana.”

Winga huyo ameonekana wazi kuongezeka misuli katika picha za hivi karibuni za mazoezi.

Kocha Mikel Arteta pia alimpongeza Ijumaa, amesema: “Nadhani amekuwa thabiti sana, mwenye kiwango kizuri mara kwa mara, kama ilivyo kwa wachezaji wote wa mbele. Wote wamechangia vizuri msimu huu hadi sasa, iwe wanaanza au wanaingia kama wachezaji wa kutokea benchini.

“Hicho ndicho tunachohitaji. Popote tunapowaweka, wataleta sifa tofauti kwa timu, lakini nadhani wako katika wakati mzuri sana.”

Arsenal inaingia nusu ya pili ya msimu ikiwa juu kwenye msimamo wa Ligi Kuu England. Kabla ya mechi ya Jumamosi dhidi ya Bournemouth, Arsenal ilikuwa inaongoza msimu wa ligi hiyo kwa tofauti ya pointi nne.