Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Garnacho kuwanunulia msosi mastaa wenzake Man United

New Content Item (1)
New Content Item (1)

Muktasari:

  • Winga huyo wa Kiargentina alitoka kabisa uwanjani baada ya kufanyiwa mabadiliko katika mechi ya wiki iliyopita dhidi ya Ipswich Town na hakuonekana kwenye benchi kipindi chote cha pili.

MANCHESTER, ENGLAND: KINDA wa Manchester United, Alejandro Garnacho atawanunulia chakula cha usiku wachezaji wenzake kama “adhabu” kutokana na kitendo chake cha kuondoka kabisa Old Trafford baada ya kutolewa kwenye mechi.

Winga huyo wa Kiargentina alitoka kabisa uwanjani baada ya kufanyiwa mabadiliko katika mechi ya wiki iliyopita dhidi ya Ipswich Town na hakuonekana kwenye benchi kipindi chote cha pili.

Baada ya mechi, Amorim alifichua kwamba alizungumza na Garnacho, ambaye tayari msimu huu walishawahi kutibuana na kumwondoa kikosini kabla ya Krismasi mwaka jana.

Lakini, Garnacho, 20, alikwenda kuonana na kocha wake Amorim na kumwambia atanunua chakula cha usiku kwa wachezaji wote wa timu hiyo kama njia ya kuomba radhi na kwamba sio adhabu ya klabu.

Amorim alisema: “Kilikuwa kituko kwa sababu siku iliyofuatia alikuja ofisini kwangu. Nilifanya uchunguzi na kugundua kwamba alikwenda vyumbani kubadilisha nguo kwa sababu alikuwa amelowa kwa mvua. Alitazama mechi akiwa kwenye eneo jingine, hakuwapo kwenye benchi, lakini mechi ilipomalizika alikuwapo na baadaye akaondoka kwenda nyumbani.

“Hakukuwa na tatizo, lakini nilimwambia hapa Manchester United kila kitu ni muhimu na taswira ya klabu kubwa ni kitu muhimu kwelikweli. Atakwenda kuwanunua chakula cha usiku wachezaji wenzake, ni hivyo.”

Garnacho aliwekwa kando kwenye kikosi sambamba na Marcus Rashford katika mechi ya Manchester derby, Desemba mwaka jana kutokana na tatizo la kinidhamu.

Baadaye kocha Amorim alimrudisha kikosini Garnacho, lakini katika mechi hiyo ya Ipswich Town alimtoa baada ya beki wa pembeni, Patrick Dorgu kuonyeshwa kadi nyekundu. Man United ilishinda 3-2.