Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Fernandes abakiza wiki moja kuamua

Muktasari:

  • Man United imepanga kufanya mabadiliko makubwa kwenye kikosi katika dirisha hili la uhamisho wa majira ya kiangazi na Fernandes alisema baada ya mechi ya kipigo kwenye fainali ya Europa League kwamba atajua kama timu hiyo itaamua kumpiga bei.

MANCHESTER, ENGLAND: NAHODHA wa Manchester United, Bruno Fernandes ameripotiwa kwamba amepanga hadi wiki ijayo atatoa uamuzi kama anataka kuachana na miamba hiyo ya Old Trafford baada ya kuwekewa mezani dili la Pauni 200 milioni kutoka klabu ya Al-Hilal ya Saudi Pro League.

Man United imepanga kufanya mabadiliko makubwa kwenye kikosi katika dirisha hili la uhamisho wa majira ya kiangazi na Fernandes alisema baada ya mechi ya kipigo kwenye fainali ya Europa League kwamba atajua kama timu hiyo itaamua kumpiga bei.

“Kama klabu itaona ni wakati wa kuachana na mimi kwa sababu itahitaji pesa au vinginevyo itaeleweka,” alisema na kuongeza. “Soka wakati mwingine ipo hivyo. Siku zote nimekuwa wazi, kwamba nitaendelea kuwa hapa hadi hapo klabu itakaposema ni muda wa kuondoka. Nataka kufanya zaidi na kuirudisha klabu kwenye makali yake kama zamani.”

Kwa mujibu wa Daily Mail, Al-Hilal imeonyesha dhamira ya kumsajili kiungo huyo wa Ureno na ipo tayari kuipa Man United ofa ya Pauni 100 milioni. Na kinachoripotiwa mkataba wake utakuwa wa miaka mitatu na mshahara wa Pauni 700,000 kwa wiki.

Kilichoelezwa ni kwamba Al-Hilal itapeleka ofa rasmi siku chache zijazo na itatoa hadi mwishoni mwa Mei kufahamu uamuzi wa mwisho kabla ya klabu hiyo kwenda kwenye fainali za Kombe la Dunia la Klabu mwezi ujao huko Marekani.

Licha ya Man United kuwa na msimu wa hovyo, Fernandes alikuwa bora uwanjani akichangia mabao 38 katika mechi 56 alizocheza kwenye michuano yote. Jambo hilo lilimfanya kocha wa Man United, Ruben Amorim kuhitaji nahodha wake huyo kubaki Old Trafford.

“Nadhani inaeleweka kuelewa hizi tetesi za usajili kwa sababu ya jinsi anavyocheza,” alisema Amorim mwanzoni mwa mwezi huu na kuongeza. “Ni mchezaji wa kiwango cha juu na sisi tunahitaji wachezaji bora.

“Ni kiongozi, nahodha. Ni kawaida kuona watu wanamtaka Bruno, lakini sisi tunataka abaki. Ni mmoja wa wachezaji bora duniani.” Hata hivyo, baada ya kipigo cha bao 1-0 kwenye fainali ya Europa League na kuifanya Man United kushindwa kupata Pauni 100 milioni kwa kufuzu kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao, hilo linaweza kuwasukuma kuuza wachezaji wao ili kupasa pesa za usajili.