Wydad AC yatambulisha wapya watatu, Aziz Ki ndani

Muktasari:
- Kwa mujibu wa taarifa ya klabu hiyo ya Morocco ni kwamba nyota hao wametua ikiwa ni juhudi za kuimarisha kikosi cha timu ya kwanza cha timu hiyo, kwa ajili ya maandalizi ya mashindano yajayo.
KLABU ya Wydad imewatambulisha nyota watatu wapya, akiwamo aliyekuwa kiungo mshambuliaji wa Yanga, Stephane Aziz Ki waliojiunga na timu hiyo inayojiandaa na Michuano ya Kombe la Dunia kwa Klabu 2025 itakatofanyikia Marekani.
Kwa mujibu wa taarifa ya klabu hiyo ya Morocco ni kwamba nyota hao wametua ikiwa ni juhudi za kuimarisha kikosi cha timu ya kwanza cha timu hiyo, kwa ajili ya maandalizi ya mashindano yajayo.
Mbali na Aziz KI, taarifa hiyo umewataja wachezaji wengine ni; Nour El-Din Amrabat na Hamza Henouri.
Tukiwatakia kila la heri na mafanikio pamoja na timu.
Na uongozi wa Klabu ya Wydad wa michezo hauwezi ila kutoa shukrani kwa mashabiki wake wote kwa msaada wao wa kudumu na kwa kulikuza nembo ya Wydad daima. Ninyi ni moyo wa timu hii nyekundu. Imesomeka taarifa hiyo.
Aziz KI aliyeitumikia Yanga kwa misimu mitatu tangu 2022 aliposajiliwa kutoka Aaec Mimosas ya Ivory Coast, inadaiwa ameuzwa Wydad kwa dili la Sh 2 Bilioni.