Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Familia ya Martinez yafunguka kufeli dili la Man United

Muktasari:

  • Martinez, 33, alikuwa kwenye rada za Man United, ambayo ilikuwa sokoni kusaka kipa mpya kabla ya dirisha halijafungwa, Jumatatu ya Septemba 1.

BUENOS AIRES, ARGENTINA: FAMILIA ya Emiliano Martinez imefunguka kwa mara ya kwanza baada ya kipa huyo wa Aston Villa kushindwa kukamilisha dili lake la kujiunga na Manchester United kwenye siku ya mwisho ya kufungwa kwa usajili.

Martinez, 33, alikuwa kwenye rada za Man United, ambayo ilikuwa sokoni kusaka kipa mpya kabla ya dirisha halijafungwa, Jumatatu ya Septemba 1.

Lakini, Man United kwenye rada zake kulikuwa na jina la kipa mwingine, Senne Lammens wa Royal Antwerp, ambaye ndiye ilimsajili siku hiyo na hivyo kuachana na mpango wa kunasa huduma ya Martinez. Kocha wa Man United , Ruben Amorim aliona ni vyema kumchukua Lemmens, 23, kwa sababu ada yake ilikuwa rahisi, Pauni 18.2 milioni na nyongeza ya Pauni 3.5 milioni endapo atafanya vyema huko Old Trafford.

Hiyo licha ya kwamba Martinez alikuwa ameshafikia makubaliano binafsi na Man United, hivyo hiyo Septemba 1 alikuwa Villa Park akisubiri simu ya mabosi wa Old Trafford, ambayo haikuita. Na kinachoelezwa ni kwamba kipa huyo wa zamani wa Arsenal alimpigia simu beki wa Man United, ambaye ni Muargentina mwenzake, Lisandro Martinez ampigie debe. Lakini, mpango ulikwama na Martinez alisaini mkataba mpya Villa Park utakaofika tamati 2029.

Kaka yake Martinez, Alejandro na baba yake Alberto, walibainisha hilo lililotokea kuhusiana na uhamisho wa Man United kukwama.

"Niliambiwa Emi amejitolea mengi kama profesheno na mtu wa kawaida, wamempenda kwa kile anachofanya uwanjani," alisema Alejandro.

"Huu ni uamuzi uliofanywa na mabosi wa klabu. Uhamisho haukutokea na kila kitu kilikuwa biashara. Kila kitu kilimalizwa vizuri."

Kaka huyo alipuuzia pia taarifa kwamba kipa Martinez ametibuana na kocha wa Aston Villa, Unai Emery, aliposema: "Emi hajawahi kulumbana na Unai." Na kuongeza: "Pale Aston Villa, yeye ni Diego (Maradona) wa Napoli. Amejitolea mengi Villa, kama Kun (Aguero) alivyofanya (Manchester) City, kama Leo (Messi) alivyofanya Barca. Ni wachezaji magwiji, hivyo ni ngumu kusikia kwamba yeye ni wa ziada Aston Villa."

Baba yake, Alberto aliongeza: "Hii ni kali, hiki ni kiwanda na viwanja vinahitaji waajitiwa. Yeye ni mwajiriwa, hivyo kiwanda hakiwezi kumruhusu aondoke. Ni suala la biashara. Leo imeshindika, kesho itatokea."