Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Erik ten Hag ajibu kwa uchungu

TEN Pict

Muktasari:

  • Hilo limekuja baada ya kocha huyo wa zamani wa Manchester United kufutwa kazi baada ya kuingoza Leverkusen kwenye mechi mbili tu za Bundesliga.

MUNICH, UJERUMANI: KOCHA Erik ten Hag kwa hasira amewashutumu mabosi wa Bayer Leverkusen kwamba hawakuwahi kuwa na imani juu yake wakati wanamkabidhi majukumu ya kuinoa timu hiyo ya Bundesliga.

Hilo limekuja baada ya kocha huyo wa zamani wa Manchester United kufutwa kazi baada ya kuingoza Leverkusen kwenye mechi mbili tu za Bundesliga.

Ten Hag, 55, alibamba dili la kwenda kupiga kazi kwenye klabu hiyo ya Ujerumani kurithi mikoba ya Xabi Alonso, aliyemtikia zake Real Madrid mwishoni mwa msimu uliopita.

Na uvumi wa kibarua cha kocha huyo kuwa kwenye mashaka makubwa uliibuka wikiendi wakati Leverkusen iliporuhusu mabao kwenye dakika za mwisho na kupata sare ya 3-3 dhidi ya Werder Bremen. Matokeo hayo yaliimaanisha Leverkusen kuvuna pointi moja tu kwenye mechi mbili za Bundesliga na hivyo Ten Hag akajikuta akipoteza ajira yake.

Mabosi wa Leverkusen waliamua kuachana na Ten Hag baada ya kutangaza kumpiga chini Jumatatu kwenye taarifa iliyotolewa kwenye tovuti ya klabu.

“Kocha mpya anahitaji muda wa kufanya mambo yake na kutengeneza vitu vyake, kuunda kikosi ili icheze kwa staili yake,” alisema.

“Nilianza hii kazi kwenye klabu hii nikiwa na nguvu kubwa, lakini kwa bahati mbaya uongozi umeshindwa kunipa muda na kuniamini, najutia sana. Huu uamuzi wa uongozi wa Bayer Leverkusen kuachana na mimi umenishangaza sana. Kuachana na kocha baada ya mechi mbili za ligi.

“Klabu ambazo ziliweka imani juu yangu zilipata zawadi ya kubeba mataji. Mwisho, nitawashukuru tu Bayer Leverkusen kwa sapoti yao na kitakia kikosi na kocha mpya mafanikio mengi katika sehemu iliyobaki ya msimu.”