Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

EPL London Derby kitawaka

Muktasari:

  • Ukiweka kando kipute hicho cha Emirates, kasheshe jingine litakuwa huko City Ground wakati Nottingham Forest inayosaka tiketi ya kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao itakuwa nyumbani kukipiga na Manchester United.

LONDON, ENGLAND: MCHAKAMCHAKA wa Ligi Kuu England umerudi upya baada ya kupisha mechi za kimataifa, huku masikio na macho ya wengi yatakuwa huko Emirates kwenye kipute cha London derby, Arsenal itakapomalizana na Fulham, Aprili 1.

Ukiweka kando kipute hicho cha Emirates, kasheshe jingine litakuwa huko City Ground wakati Nottingham Forest inayosaka tiketi ya kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao itakuwa nyumbani kukipiga na Manchester United.

Kwenye karatasi mechi ya Arsenal na Fulham inaonekana ni kama ya upande mmoja kutokana na takwimu za mechi ya miamba hiyo inapokabiliana, ambapo kwenye mechi 35 zilizochezwa, Arsenal imeshinda 23, wakati Fulham nne tu. Katika mechi ilizoshinda Arsenal, 11 nyumbani na 12 ugenini, wakati Fulham yenyewe haijawahi kushinda ugenini ilipocheza na The Gunners, huku mechi nane baina yao, zilimalizika kwa sare.

Kwenye mechi ya Forest na Man United, takwimu zipo upande wa miamba ya Old Trafford, lakini kwa kiwango cha kikosi hicho cha kocha Ruben Amorim kwa sasa ndicho kinacholeta shaka kubwa kwenye mechi hiyo, kwa sababu inakwenda kucheza ugenini dhidi ya Forest iliyo kwenye kiwango bora kabisa.

Kwenye mechi za Ligi Kuu England, Forest na Man United zimekutana mara 15, ambapo sare ni mbili tu, huku Foest ikishinda tatu, mara moja nyumbani City Ground na mbili ugenini, wakati Man Unitd yenyewe imeshinda 10, sita nyumbani na nne ugenini, ambako itakwenda kukipiga Jumanne, Aprili 1.

Mchezo wa tatu utakaofanyika Aprili 1, utakuwa huko Molineux, ambapo Wolves itakuwa na kibarua kizito mbele ya West Ham United. Wolves na West Ham zinapokutana shughuli ni pevu, ambapo katika mechi 17 ilizokutana kwenye Ligi Kuu England, moja ilimalizika kwa sare, huku Wolves ikishinda saba, nne nyumbani na tatu ugenini, wakati West Ham imeshinda tisa, sita nyumbani na tatu ugenini. Patachimbika.

Jumatano, Aprili 2 itashuhudia mechi sita, ikiwamo kipute cha Merseyside derby, ambapo Liverpool itakuwa nyumbani uwanjani Anfield kukipiga na Everton katika moja ya mechi za kibabe sana. Kwenye Ligi Kuu England, Liverpool na Everton, ambao ni mahasimu wakubwa, walikutana mara 65, ambapo 26 zimemalizika kwa sare, huku vijana wa Arne Slot wakishinda 28, mara 17 nyumbani na 11 ugenini, wakati Everton ya kocha David Moyes imeshinda 11, mara nane nyumbani na tatu ugenini.

Bournemouth itakuwa nyumbani kucheza na Ipswich Town, wakati Brighton itakuwa na kasheshe zito mbele ya Aston Villa ya Unai Emery, huku Newcastle United itaonyesha ubabe na Brentford na Southampton itacheza na Crystal Palace.

Manchester City, ambao ni mabingwa watetezi wa Ligi Kuu England, watakuwa Etihad kucheza na Leicester City.

Man City na Leicester City zimekutana mara 25 kwenye EPL, ambapo mara mbili zilimalizika kwa sare, huku vijana wa Pep Guardiola wakishinda 16, mara saba nyumbani na tisa ugenini, wakati Leicester City imeshinda saba, mbili nyumbani na tano ugenini. Patachimbika.

Alhamisi, Aprili 3, kitapigwa kipute cha maana kabisa cha London derby, wakati Chelsea itakapokuwa nyumbani kukipiga na Tottenham Hotspur. Chelsea ya kocha Enzo Maresca inahitaji kushinda mchezo huo ili kuendelea kufukuzia tiketi ya kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao, huku Spurs ikipambana kuhakikisha haimalizi msimu huu vibaya.

Kwenye takwimu, zinaonyesha Chelsea na Spurs zimekutana mara 65 kwenye Ligi Kuu England, ambapo mara 21 zilitoka sare, huku The Blues ikishinda 36, mara 20 nyumbani na 16 ugenini, wakati Spurs imeshinda nane, mara nane nyumbani na saba ugenini.

Hiyo ina maana, Spurs itakwenda Stamford Bridge kujaribu kusaka ushindi wao wa pili kwenye Ligi Kuu England, huku The Blues ikisaka ushindi wake wa 21 uwanjani hapo.