Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Enzo Maresca, Chelsea lolote linaweza kutokea

MARESCA Pict

Muktasari:

  • Kocha huyo Muitaliano hakuonekana kwenye mkutano wa waandishi wa habari baada ya mechi ya sare ya mabao 2-2 dhidi ya Bournemouth Jumanne, huku klabu ikieleza kuwa alikuwa amepata homa.

LONDON, ENGLAND: KOCHA wa Chelsea, Enzo Maresca yuko tayari kujiuzulu kuifundisha timu hiyo  kufuatia mgogoro mkubwa uliotokea kati yake na bodi ya klabu hiyo.

Kocha huyo Muitaliano hakuonekana kwenye mkutano wa waandishi wa habari baada ya mechi ya sare ya mabao 2-2 dhidi ya Bournemouth Jumanne, huku klabu ikieleza kuwa alikuwa amepata homa.

Hata hivyo, tovuti ya The Sun, imebaini kuwa kutohudhuria mkutano huo ulikuwa ni uamuzi wa  makusudi wa Maresca na kwamba hakukuwa na tatizo lolote la kiafya lililomkuta.

Inaelezwa, Maresca alitaka kutafakari kwa kina mustakabali wake ndani ya klabu hiyo, huku akifikiria uwezekano wa kuondoka mwenyewe katika viunga hivyo vya Stamford Bridge.

MARE 01

Hadi sasa bado kocha huyu hajafikia uamuzi wa mwisho juu ya mustakabali wake.

SunSport imeripoti kuwa Maresca aliyesaini mkataba wa miaka mitano alipojiunga na Chelsea Juni 2024, anaheshima kubwa sana kwa Chelsea na mashabiki wake.

Moja kati ya sababu zinazodaiwa kumfanya afikirie kuondoka mwenyewe bila ya kufukuzwa ni shinikizo kubwa la matarajio kutoka kwa mashabiki wa timu hiyo ambalo linatokana na mafanikio ya klabu hiyo katika kipindi cha miaka 20 iliyopita.

Imeelezwa kuwa Maresca amefikia hatua ambayo hawezi tena kuficha hisia zake za kutoridhika na kile kinachoendelea katika timu ambapo anaamini hapewi uhuru wa kufanya kazi yake vile ambavyo anahitaji.

Maresca, ambaye amewapa wachezaji wake mapumziko ya siku mbili, huenda pia asiwe katika benchi la ufundi katika mchezo wa Jumapili dhidi ya Manchester City, ambapo huenda akawa amejiuzulu hadi kufikia wakati huo.

Katika mechi dhidi ya Bournemouth, mashabiki wa Chelsea waliokaa katika jJukwaa la Matthew Harding walikuwa wakiimba wakisema Maresca, “hujui anachofanya,” mara baada ya kumtoa nyota wao Cole Palmer.

MARE 02

Licha ya kwamba kulikuwa na takribani dakika 30 bado za kucheza, kelele za kuzomea zilisikika kote katika dimba la Stamford Bridge.

Kikosi cha Maresca chenye wastani mdogo zaidi wa umri katika Ligi Kuu England msimu huu, kimeendelea kupoteza pointi licha ya kuwa ndani ya nafasi tano za juu.

Chelsea sasa imeangusha jumla ya pointi 15 na 13 kati ya hizo ni zile za mechi ilizocheza kwenye uwanja wake wa nyumbani.

Kwa sasa ipo nafasi ya tano kwenye msimamo wa Ligi Kuu, ikiwa nyuma kwa pointi 15 dhidi ya vinara Arsenal.

Mmiliki mwenza wa Chelsea, Behdad Eghbali alitokea uwanjani huku uso wake ukiwa umefura kwa hasira baada ya kumalizika kwa mechi dhidi ya Bournemouth.

Endapo Chelsea itapoteza dhidi ya Manchester City inayowania ubingwa, kisha ikashindwa kushinda dhidi ya majirani zao Fulham siku tatu baadaye, inaweza kujikuta katikati ya msimamo wa ligi.

Kabla ya Krismasi, Maresca alikuwa akitajwa kama mrithi anayeweza kuchukua mikoba ya Pep Guardiola katika kikosi cha Manchester City.