Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Duh! Eti avuliwe Odegaard avae Rice

ODE Pict

Muktasari:

  • Beki wa zamani wa Arsenal, Adams alisema mwanzoni mwezi huu kwamba kocha Mikel Arteta anapaswa kumvua kitambaa cha unahodha Odegaard na badala yake ampe Declan Rice kama kweli timu hiyo ina ndoto za kunyakua ubingwa wa Ligi Kuu England.

LONDON, ENGLAND: STAA wa zamani wa Arsenal, Anders Limpar ameungana na gwiji wa klabu hiyo, Tony Adams kutaka kiungo Martin Odegaard avuliwe kitambaa cha unahodha wa klabu hiyo.

Beki wa zamani wa Arsenal, Adams alisema mwanzoni mwezi huu kwamba kocha Mikel Arteta anapaswa kumvua kitambaa cha unahodha Odegaard na badala yake ampe Declan Rice kama kweli timu hiyo ina ndoto za kunyakua ubingwa wa Ligi Kuu England.

Kiungo huyo wa Norway, Odegaard alichaguliwa kuwa nahodha wa Arsenal katika msimu wa 2022/23 na katika kipindi chake alishuhudia kikosi hicho kikimaliza msimu wa ligi kwneye nafasi ya pili kwa misimu mitatu mfululizo, lakini hakuna taji lolote kubwa walilobeba.

Na sasa Limpar, ambaye alibeba ubingwa na Arsenal mwaka 1991, alisema Odegaard ni mchezaji mahiri, lakini Limpar hakutaka kupingana na Adams juu ya mchezaji gani awe kiongozi.

“Kama Tony Adams anasema Declan Rice anapaswa kuwa nahodha wa Arsenal nitaunga mkono hilo,” alisema Limpar, 59.

“Siwezi kusema chochote kumpinga nahodha wangu, hakika. Ni mmoja wa manahodha bora kwenye mchezo wa soka na amebeba mataji mengi. Ninachosema wala sio muhimu, kwamba niwe hapa nisema Arsenal imbadili nahodha na kumpa Declan Rice. Lakini, kama Tony Adams anasema hivyo kwamba Declan Rice anapaswa kuwa nahodha, nitaunga mkono.”

Hata hivyo, Limpar alisema haoni kama nahodha wa zamani wa West Ham, Rice anataka kuwa nahodha wa timu hiyo ya Arsenal, ambayo imeanza vizuri kabisa kwenye Ligi Kuu England msimu huu baada ya ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Manchester United na ule wa mabao 5-0 dhidi ya Leeds United. Kesho, Jumapili itakipiga na Liverpool huko uwanjani Anfield.