Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

DR Congo kwenye ramani ya soka la Dunia baada ya miongo mitano

Muktasari:

  • Ushindi huo wa kihistoria umepatikana baada ya vijana wa "The Leopards" kupata ushindi mwembamba lakini wa thamani wa bao 1-0 dhidi ya timu ngumu ya Jamaica. Shujaa wa mchezo huo hakuwa mshambuliaji, bali ni beki imara Alex Tuanzebe, ambaye aliunganisha mpira wavuni na kuamsha shangwe zisizo na kifani kwa Wakongo wote na Waafrika kiujumlaDuniani.

KINSHASA, DR Congo:  Baada ya kusubiri kwa zaidi ya nusu karne, hatimaye ndoto ya mamilioni ya Wakongo imetimia. Timu ya Taifa ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) imefanikiwa kufuzu rasmi kushiriki michuano ya Kombe la Dunia ya FIFA 2026, itakayofanyika kwa pamoja nchini Marekani, Mexico, na Canada.

Ushindi huo wa kihistoria umepatikana baada ya vijana wa "The Leopards" kupata ushindi mwembamba lakini wa thamani wa bao 1-0 dhidi ya timu ngumu ya Jamaica. Shujaa wa mchezo huo hakuwa mshambuliaji, bali ni beki imara Alex Tuanzebe, ambaye aliunganisha mpira wavuni na kuamsha shangwe zisizo na kifani kwa Wakongo wote na Waafrika kiujumlaDuniani.


Safari ya Tuanzebe: Kutoka England hadi shujaa wa Taifa

Mafanikio haya yanatoa picha ya kipekee kuhusu safari ya Alex Tuanzebe. Beki ambaye amewahi kukipiga katika klabu ya Manchester United, hapo awali aliwakilisha timu za vijana za taifa la England. Hata hivyo, mwaka 2024 alifanya maamuzi magumu na ya kishujaa ya kurejea katika asili yake na kuanza kuitumikia DR Congo.

Mchezo wake wa kwanza ulikuwa dhidi ya miamba ya Afrika, Senegal, ambapo alionyesha uwezo mkubwa wa uongozi safu ya ulinzi. Ndani ya miaka miwili tu tangu aanze kuvaa jezi ya Leopards, Tuanzebe amekuwa muhimili mkuu na sasa ameweka jina lake kwenye vitabu vya kumbukumbu kwa kuifungia nchi yake bao lililovunja mwiko wa miongo mitano.


Kuziba Pengo la Miaka 52

Mara ya mwisho kwa DR Congo (wakati huo ikijulikana kama Zaire) kushiriki Kombe la Dunia ilikuwa mwaka 1974 kule nchini Ujerumani Magharibi. Tangu wakati huo, kizazi baada ya kizazi kimeshindwa kufikia hatua hiyo, jambo ambalo liliacha jeraha la kimichezo kwa nchi hiyo inayopenda soka kwa dhati.

"Huu ni wakati wa kipekee kwa taifa letu. Tumesubiri kwa miaka 52, na leo tumewathibitishia ulimwengu kuwa DR Congo ni taifa la soka," walisikika mashabiki wakishangilia mitaani.

Kwa ushindi huu, DR Congo inaungana na mataifa mengine makubwa duniani kuelekea Amerika ya Kaskazini mnamo June, 2026. Chini ya uongozi wa benchi la ufundi lililojipanga na safu ya ulinzi inayoongozwa na Tuanzebe, Leopards hawaendi tu kama washiriki, bali kama washindani wanaotaka kufuta kumbukumbu mbaya za mwaka 1974 na kuandika historia mpya kwa soka la Afrika.

DR Congo Kombe la Dunia ipo grupu K pamoja na Ureno, Uzbekistan na Colombia