Djokovic bado hajamaliza

Muktasari:
- Ni Mserbia Novak Djokovic aliyekuwa na ndoto hiyo kubwa kwa muda mrefu ya kushinda mataji yote makubwa ya tenisi duniani, awali akiwa na mataji yote manne (Grand Slam) ambayo ni Australia, Rolland Garros, Wimbledon na lile la US Open.
HAIKUWA rahisi kutimiza ndoto ya muda mrefu, hadi alipomshinda mpinzani wake mkubwa kwa sasa kwenye tenisi, Carlos Alcaraz katika fainali ya Olimpiki Ufaransa.
Ni Mserbia Novak Djokovic aliyekuwa na ndoto hiyo kubwa kwa muda mrefu ya kushinda mataji yote makubwa ya tenisi duniani, awali akiwa na mataji yote manne (Grand Slam) ambayo ni Australia, Rolland Garros, Wimbledon na lile la US Open.
Nyota huyo alibakiza taji moja kubwa pekee la Olimpiki ambalo tangu 2008 pale Beijing, ikafuata Londo 2012, Rio 2016 na Tokyo 2020, Kote aliishia kuchapwa na wapinzani ambao walienda kubeba taji hilo ambao ni Rafael Nadal, Andy Murray na Alexander Zverev waliochukua mara nne zilizopita.
Djokovic ambaye amesisitiza bado hajamaliza akiwekea lengo la kushinda na taji lijalo la 2028 nchini Marekani, ameungana na Nadal, Steff Graff, Andre Agassi na Serena Williams waliokuwa wameshinda mataji yote manne ya mwaka pamoja na hili la Olimpiki.