Dili la Haaland lazipasua kichwa Barcelona, Manchester City

Thursday April 08 2021
haaland pc

MANCHESTER City na Barcelona zimeendelea kupambana kuhakikisha zinaipata saini ya staa wa Borussia Dortmund na timu ya taifa ya Norway, Erling Braut Haaland, 20, dirisha lijalo la majira ya kiangazi.

Hata hivyo, ugumu unatoka kwa mabosi wa Borussia Dortmund ambao mtendaji wao mkuu, Hans-Joachim Watzke amesisitiza hawana mpango wa kumuuza fundi huyo dirisha lijalo kwa sababu wana mipango naye kwa msimu ujao.

Hii imeibua vuta nikuvute baina ya wawakilishi wa Haaland wakiongozwa na Mino Raiola dhidi ya mabosi wa Dortmund. Wakati Dortmund inakataa kumuuza Haaland, tayari Raiola na baba mzazi wa fundi huyo wamefanya vikao na timu zilizoonyesha nia ya kumhitaji.

Man City huenda ikaandaa kiasi kisichopungua Pauni 100 milioni ili kufanikisha dili la fundi huyo.

Dortmund inasita kumuuza Haaland kwa sababu inahofia kikosi chao kuyumba sana kwani imekubali pia kusikiliza ofa kwa ajili ya timu zinazohitaji huduma ya winga wao na timu ya taifa ya England, Jadon Sancho, mwisho wa msimu.

Advertisement