Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

De Ligt: Amorim? tupo naye

DE LIGHT Pict

Muktasari:

  • Presha kwa kocha huyo ilishuka Jumamosi iliyopita baada ya kikosi cha Man United kupata ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Burnley, bao la ushindi likifungwa kwa mkwaju wa penalti dakika ya 97 na nahodha Bruno Fernandes.

MANCHESTER, ENGLAND: BEKI wa kati wa Manchester United, Matthijs de Ligt amesisitiza wachezaji wa timu hiyo wanampa sapoti kubwa Kocha Ruben Amorim na wanamtaka abaki.

Presha kwa kocha huyo ilishuka Jumamosi iliyopita baada ya kikosi cha Man United kupata ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Burnley, bao la ushindi likifungwa kwa mkwaju wa penalti dakika ya 97 na nahodha Bruno Fernandes.

Huo ulikuwa ushindi wa kwanza wa Man United Ligi Kuu England msimu huu baada ya kutokea kutupwa nje ya Kombe la Ligi na klabu ndogo ya Grimsby kwa mikwaju ya penalti katikati ya wiki iliyopita.

Jambo hilo lilimfanya Amorim kuwa kwenye presha kubwa na hofu angefunguliwa mlango wa kutokea, lakini De Ligt alisema wachezaji bado wana imani kubwa na kocha huyo na wao ndio wanapaswa kubebeshwa lawama kwa kuanza vibaya msimu huu.

Alipoulizwa kama wachezaji wa Man United wanataka Amorim abaki, De Ligt alisema: “Ndiyo, bila shaka. Nina maana, kama mchezaji, ninawajibika na matokeo. Siku zote amekuwa akizungumzwa kocha, lakini nadhani kama wachezaji, tulitazamana machozi baada ya ile mechi ya Grimsby na kuambizana, ‘Jamani, hiki kiwango cha wiki hii hakikubaliki’.

“Ilikuwa kweli, nadhani ni kitu kibaya kusema ni kosa la kocha. Hilo lipo juu yetu na tunatambua hilo. Hivyo, ni wazi, bado tunampa sapoti na tutapambana kwa ajili yake. Nadhani mambo yatakuwa vizuri zaidi ya baada ya mechi hii.”

Man United itakabiliwa na mitihani miwili itakaporejea mzigoni baada ya mapumziko ya mechi za kimataifa na itakwenda Etihad kukipiga na mahasimu wao Manchester City na baada ya hapo, itarudi Old Trafford kukabiliana na Chelsea.