Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Dani Alves ashinda rufaa yake, afutiwa kesi ya kubaka

Muktasari:

  • Staa huyo wa zamani wa Barcelona, alihukumiwa kifungo cha miaka minne na nusu jela baada ya kukutwa na hatia ya kumbaka mwanamke mmoja kwenye kumbi moja ya starehe za usiku huko Barcelona, Desemba 2022.

MADRID, HISPANIA: BEKI wa Kibrazili, Dani Alves amefutiwa kesi ya kubaka iliyokuwa ikimkabili baada ya kushinda rufaa yake.

Staa huyo wa zamani wa Barcelona, alihukumiwa kifungo cha miaka minne na nusu jela baada ya kukutwa na hatia ya kumbaka mwanamke mmoja kwenye kumbi moja ya starehe za usiku huko Barcelona, Desemba 2022.

Kwenye hukumu hiyo, Alves alitakiwa pia kumlipa fidia ya Pauni 130,000 mwanamke huyo na asimsogelee kabisa kwa kipindi cha miaka tisa na nusu. Lakini, Alves, ambaye alikuwa nje kwa dhamana tangu Machi mwaka jana, alikata rufaa na kudai kwamba tukio la ngono lilikuwa la kutunga.

Hivyo, Mahakama Kuu ya Catalan ilimfutia mashtaka hayo Alves baada ya kukosekana kwa ushahidi wa kutosha juu ya namna tukio lenyewe lilivyotokea baada ya majaji wanne, Maria Angels Vivas, Roser Bach, Maria Jesus Manzano na Manuel Álvarez kuona makosa makubwa yaliyofanyika kwenye mahakama ya mwanzo ya Barcelona.

Mke wa Alves, mwanamitindo Joana Sanz amekuwa bega kwa bega na mumewe kwa kipindi chote hicho baada ya kubadili mawazo ambapo awali alikuwa akitaka kuomba talaka baada ya mumewe kufunguliwa mashtaka ya kubaka.

Alves aliondoshwa kwenye klabu yake ya UNAM Pumas ya huko Mexico baada ya kukamatwa Barcelona mwanzoni mwa mwaka jana wakati alirudi Hispania kuhudhuria maziko ya mama mkwe. Alikaa rumande kwa zaidi ya miezi 14 kabla ya kutolewa kwa dhamana ya masharti ya kutotoka nje ya Hispania na alikuwa na kazi ya kwenda kusaini mahakamani kila Ijumaa.