Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Dah! Merino atibua hesabu huko Arsenal

MERINO Pict

Muktasari:

  • Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 29 aliachwa nje ya kikosi cha Arsenal kilichoshinda Leeds United kwa mabao 4-0 Jumamosi, huku kocha Mikel Arteta akithibitisha kuwa alikuwa na tatizo la mguu. Sasa klabu imethibitisha kuwa Merino atakuwa nje kwa kipindi kirefu na atalazimika kufanyiwa upasuaji.

LONDON, ENGLAND: STAA wa Arsenal, Mikel Merino anatarajiwa kuwa nje ya uwanja muda mrefu kwa jeraha la mguu linalohitaji upasuaji.

Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 29 aliachwa nje ya kikosi cha Arsenal kilichoshinda Leeds United kwa mabao 4-0 Jumamosi, huku kocha Mikel Arteta akithibitisha kuwa alikuwa na tatizo la mguu. Sasa klabu imethibitisha kuwa Merino atakuwa nje kwa kipindi kirefu na atalazimika kufanyiwa upasuaji.

Taarifa ya klabu iliseomeka:”Baada ya kupata jeraha la mguu kuelekea mwisho wa mechi yetu dhidi ya Manchester United mnamo Januari 25, vipimo na tathmini za kitaalamu zimethibitisha kuwa Mikel Merino ana jeraha la mfupa kwenye mguu wake wa kulia.

“Mikel atafanyiwa upasuaji katika siku chache zijazo kisha aanze mpango wake wa kupona na kurejea.

“Anatarajiwa kuwa nje ya uwanja kwa muda mrefu, kwa lengo la kurejea mazoezini kikamilifu kabla ya msimu kumalizika.

“Kila mtu yuko makini kumsaidia Mikel kuhakikisha anarudi katika hali yake bora haraka iwezekanavyo.”

Jeraha la Merino limekuja katika wakati mbaya, hasa baada ya Arsenal kumruhusu kiungo mshambuliaji mwenzake, Ethan Nwaneri, kujiunga na Marseille kwa mkopo hadi mwisho wa msimu. Na kinachoelezwa Arsenal ilikuwa tayari kusajili mchezaji mbadala kabla ya dirisha la usajili kufungwa.

Hata hivyo, mchezaji yeyote atakayesajiliwa atalazimika kuingia moja kwa moja kikosini na kuwa na ubora wa kusaidia kuendeleza harakati za Arsenal za kutwaa ubingwa. Kwa sasa, hakuna ratiba maalum ya kurejea kwa Merino.

Akizungumza kupitia Instagram, Merino aliandika: “Ni wakati wa kusimama kidogo kutokana na jeraha la mguu. Wakati mwingine maisha huleta changamoto kama hizi wakati usiofaa.”