Dada afunguka Ronaldo kutohudhuria mazishi

Muktasari:
- Mshambuliaji wa Liverpool Jota alizikwa Jumamosi baada ya kupoteza maisha kwa ajali ya gari pamoja na mdogo wake Andre Silva Julai 3. Ibada ya mazishi iliyofanyika karibu na mji alikozaliwa Jota huko Porto, ilihudhuriwa na baadhi ya wachezaji wenzake na makocha wake.
PORTO, URENO: BAADA ya ripoti nyingi juu ya kukosekana kwa staa Cristiano Ronaldo kwenye mazishi ya Diogo Jota, hatimaye dada yake, Katia Aveiro, ameeleza ukweli kwa nini nahodha huyo wa Ureno hakuhudhuria mazishi.
Mshambuliaji wa Liverpool Jota alizikwa Jumamosi baada ya kupoteza maisha kwa ajali ya gari pamoja na mdogo wake Andre Silva Julai 3. Ibada ya mazishi iliyofanyika karibu na mji alikozaliwa Jota huko Porto, ilihudhuriwa na baadhi ya wachezaji wenzake na makocha wake.
Ronaldo, ambaye sasa anacheza soka la kulipwa Saudi Arabia akiwa na Al-Nassr, hakuwa miongoni mwa waliokuwapo katika tukio hilo.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 40 amekosolewa na baadhi ya watu kwa kufanya hivyo lakini dada yake ameweka wazi kuwa Ronaldo alifanya uamuzi huo kwa heshima kwani alihofia uwepo wake ungeteka tukio hilo.
Licha ya kukosekana ripoti zinaeleza Ronaldo aliongea na mke wa Jota na famila nzima kuipa pole na kuieleza kuwa hatokwenda kwa kuhofia watu kuhamishia mawazo kwake badala ya msibani.
Vilevile, Ronaldo aliahidi kugharamia mazishi hayo lakini vyombo mbalimbali vimezidi kuendelea kuripoti na kukosoa vikieleza staa huyo hakuwepo msibani lakini alionekana akiwa katika mapumziko sehemu za starehe jambo ambalo limemkera dada yake ambaye ametoa ya moyoni jana.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram Katia aliandika: “Baba yangu alipofariki. Mbali na maumivu ya kumpoteza, tulilazimika kukabiliana na kamera nyingi na watu walituangalia kila mahali makaburini na kila tulikokwenda. Na wakati huo mitandao haikuwa kama ilivyo sasa.”
“Muda wote wa msiba hakuthubutu kutoka katika kanisani tulipokuwa hadi muda rasmi wa kuzika ulipofika, hii ni kutokana na fujo zilizokuwepo.”
“Katika kulikuwa na marais, makocha wa timu ya taifa wa wakati huo, kama Luis Filipe Scolari, n.k. Sikumkumbuka hata mmoja wao. Na hakika walinisalimia. Maumivu yalinifanya nisiwazingatie. Hali hii huwezi kuielewa mpaka yakukute.Mtu ambaye atanitumia ujumbe kumkosoa kaka yangu kwa chochote, nitamzuia na kumpuuza kabisa.”
“Inachosha sasa. Kumekuwa na ushabiki uliopitiliza. Ukosoaji usio na msingi, nasema tena, sisi sote tuna familia. Inatia aibu sana kuona vituo vya TV/wachambuzi/mitandao ya kijamii wakisisitiza na kushikilia habari za kwanini Ronalo hajakuwepo, badala ya kuheshimu maumivu ya familia iliyovunjika kwa kupoteza ndugu wawili. Naona aibu hata kutazama. Inasikitisha.”