Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Curry ammwagia maua Lebron

Muktasari:

  • Mastaa hao wamekuwa na ubora wa muda mrefu na wameshinda mataji manne ya NBA kila mmoja wakisaka la tano, huku hivi sasa wakiwa pamoja kwenye michuano ya Olimpiki nchini Ufaransa wakiiwakilisha Marekani ambayo inapewa nafasi kubwa ya kutwaa medali ya dhahabu.

WAKATI kwenye soka kukiwa na mastaa wawili wakubwa Lionel Messi na Cristiano Ronaldo ambao wamewagawa mashabiki wa soka duniani kutokana na ubora wa muda mrefu na rekodi kibao walizoweka, ndivyo ilivyo kwa nyota wa Ligi ya Kikapu Marekani (NBA), Steph Curry na LeBron James.

Mastaa hao wamekuwa na ubora wa muda mrefu na wameshinda mataji manne ya NBA kila mmoja wakisaka la tano, huku hivi sasa wakiwa pamoja kwenye michuano ya Olimpiki nchini Ufaransa wakiiwakilisha Marekani ambayo inapewa nafasi kubwa ya kutwaa medali ya dhahabu.

Ni hapo ndipo Curry maarufu pia kama Chef anayekipiga Golden State Warriors alipoweka wazi kuwa anamkubali sana LeBron kwa kile alichofanya  kwenye mchezo wa kikapu na hasa NBA akimtaja kuwa mchezaji bora zaidi katika wale wa muda wote na pia imekuwa ni bahati kwake kucheza naye timu moja ya Marekani katika Olimpiki yake ya kwanza na mwisho.


Embiid ishu ni majeraha NBA

AKIWA na tuzo ya mchezaji mwenye thamani zaidi ‘MVP’ wa ligi msimu mmoja nyuma kabla ya uliomalizika Aprili, mwaka huu, nyota wa Philadelphia 76er, Joel Embiid amesema kama si majeraha yanayomuandama kwa kipindi fulani angekuwa mchezaji bora wa muda wote kwenye NBA.

Embiid anadai alitakiwa kuwa kwenye orodha ya majina yanayotajwa ya wachezaji bora wa muda wote kama LeBron James, Michael Jordan na wengineo na anaamini ana ubora huo, lakini kinachomuangusha ni majeraha kiasi cha kumfanya ashindwe kuwa na mwendelezo wa kufanya makubwa.

Mbali na hilo, Embiid anaamini majeraha yamesababisha ashindwe kubeba taji la NBA kitu ambacho pia kinamfanya mchezaji awe na heshima zaidi kwenye ligi hiyo, lakini kukosa pia wachezaji wenza ambao wangesaidiana kushinda mataji inachangia lengo lake lisitimie kwa sasa.


Tatum na Jaylen hakuna noma

WAKATI Boston Celtics inatwaa taji la kihistoria la 18 kwenye NBA, mchezaji aliyeshtua wengi kwa kuupiga mwingi ni Jaylen Brown mbele ya supastaa wa timu hiyo, Jayson Tatum ambaye ndiye mchezaji kinara wa timu hiyo Ukanda wa Mashariki.

Brown alitisha kwenye mechi za mtoano (playoffs) ukanda huo na kufanikiwa kushinda tuzo ya MVP wa ukanda mbele ya timu ya Indiana Pacers na kama haitoshi akabeba tena tuzo ya MVP wa fainali mbele ya Dallas Mavericks.

Hii imemfanya Tatum kumbebea bango nyota mwenzake kuwa licha ya kupitia wakati mgumu akilaumiwa kutoisaidia timu hiyo misimu ya nyuma, alipaswa kumtetea wakati wote kwani ubora wake ndio umechangia wachukue taji la 18 la NBA.


Green awapiga chini Lavine, Ingram

SUPASTAA wa Golden State Warriors, Draymond Green ni kama anajifunga kubaki ndani ya timu hiyo zaidi kufuatia kuishauri katika usajili kufanya na zaidi ya ule ambao haikutakiwa kuufanya ikiwemo kuwapiga chini baadhi ya wachezaji waliokuwa kwenye rada za timu hiyo.

Lauri Markkanen wa Utah Jazz, Brandon Ingram wa New Orleans Pelicans na Zach LaVine wa Chicago Bulls ni miongoni mwa majina ambayo yangeweza kusajiliwa na Warriors kuiongozea nguvu timu hiyo baada ya kusepa kwa Klay Thompson aliyejiunga na Dallas Mavericks.

Hata hivyo, Green alidai uamuzi huo wa mabosi kuachana na usajili wa wachezaji hao uliotokana na maoni yake, umeiepushia timu gharama kubwa za usajili kwa sasa na misimu ijayo badala yake anaamini viongozi wanatakiwa kusajili sehemu zenye shida zaidi ili kuipa nafasi timu kuendelea kuwa bora bila kuwa kwenye hatari ya hasara.