Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Crystal Palace mabingwa FA baada ya miaka 120, yazima tumaini la Man City

MABINGWA Pict

Muktasari:

  • Bao pekee la dakika ya 16 la Eberechi Eze, lilitosha kuzima ndoto hiyo ya City baada kukosa pia mataji ya Ligi Kuu England lililokwenda kwa Liverpool na Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya kutolewa mapema.

MANCHESTER, ENGLAND: WIKIENDI iliyopita Manchester City ilipoteza tumaini lao la kuondoka na walau kombe moja msimu huu baada ya kupokea kichapo cha bao 1-0 kutoka kwa Crystal Palace katika fainali ya Kombe la FA.

Bao pekee la dakika ya 16 la Eberechi Eze, lilitosha kuzima ndoto hiyo ya City baada kukosa pia mataji ya Ligi Kuu England lililokwenda kwa Liverpool na Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya kutolewa mapema.

Hata hivyo, wakati ikionekana ni mwaka wa mkosi kwa Man City, ni tofauti kwa Palace ambayo ilikuwa imechukua taji lao la kwanza baada ya miaka 120 tangu kuanzishwa kwao.

Pia ubingwa huo wa FA umeiwezesha Palace kufuzu kushiriki  Europa League msimu ujao na itakuwa ni mara yao ya kwanza kushiriki michuano ya kimataifa.

MABI 01

CITY HATIHATI UEFA

Huu unakuwa ni msimu wa wa pili kwa matajiri hao wa Jiji la Manchester kumaliza bila ya kushinda taji lolote tangu Pep Guardiola achukue mikoba ya kuinoa timu hiyo kama ilivyotokea 2016/17.

Licha ya kutochukua taji lolote, hali inaonekana kuwa mbaya kwani kuna uwezekano ikashindwa hata kufuzu Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao.

MABI 05

Hadi sasa matajiri hawa wa Jiji la Manchester wanashika nafasi ya sita wakiwa na pointi 65 tofauti ya alama moja na Aston Villa ambayo ipo kwenye nafasi ya tano ambayo timu itakayomaliza hapo inafuzu Ligi ya Mabingwa.

Hata hivyo, Man City ina faida yakuwa na mchezo mmoja mkononi ambao ikishinda itapanda nafasi ya tano kwa tofauti ya alama mbili.

MABI 02

KILICHOINGUSHA

Man City ilianza kupoteza matumaini ya kutetea ubingwa wa Ligi Kuu England baada ya kupoteza baadhi ya mechi muhimu katika vipindi tofauti tofauti wakiwamo Kevin De Bruyne, Erling Haaland, Ederson, Rodri, Jeremy Doku, Manuel Akanji, Nathan Ake, Ruben Dias na John Stones na kusababisha kuathiri kiwango chao.

Guardiola pia aliangushwa na kupoteza pointi katika mechi muhimu kama dhidi ya Arsenal, Liverpool na Manchester United na kwa kiasi kikubwa zilisababisha washuke kwenye msimamo na baada ya hapo hawakuweza tena kurudi katika vita ya kutetea taji.

MABI 06

Katika michuano mengine, Man City iliondolewa katika raundi ya tatu ya Carabao Cup na Newcastle United na walipokea kichapo cha mabao 2-1 na Ligi ya Mabingwa iliondolewa na Real Madrid, kwa jumla ya mabao 6-3.

MABI 03

REKODI

Licha ya kupoteza fanali hii wikiendi iliyopita, Guardiola amekuwa na rekodi nzuri katika michuano hii kwani ameshinda mara mbili tangu atue Man City na taji linalokumbukwa zaidi ni lile la msimu wa 2022/23 na liliwawezesha kumaliza msimu ikiwa na mataji matatu kwa pamoja.

Katika mechi ya FA juzi, kinda wa Man City kutoka akademi,  Nico O'Reilly mwenye umri wa miaka 20, aliweka rekodi ya kuwa ndiye mchezaji mdogo zaidi kucheza fainali ya Kombe la FA na kikosi hicho, tangu Matija Nastasic afanye hivyo mwaka 2013 akiwa na umri wa miaka miaka 20, siku 44.

Nico pia anakuwa ndiye mchezaji mwenye umri mdogo zaidi raia wa Uingereza kufanya hivyo tangu Tommy Caton 18 na Steve MacKenzie, 19, waweke rekodi hiyo mwaka 1981.

MABI 04

Kipa wa Palace Dean Henderson aliweka rekodi ya kuwa kipa wa kwanza kuokoa penalti katika fainali ya Kombe la FA (ndani ya muda wa kawaida) tangu Petr Cech alipofanya hivyo akiwa na Chelsea dhidi ya Portsmouth mwaka 2010.

Hii ilikuwa ni fainali ya tatu kwa Palace, mara ya kwanza ikiwa ni mwaka 1996 na ikacheza tena mwaka 2016 ambapo zote ilicheza dhidi ya Manchester United na ikapoteza.